Mafuta ni nishati muhimu sana duniani, pamoja na kuwa nishati muhimu sana duniani bado nchi zinazozalisha mafuta asilia ni nchi chache sana duniani, kiasi kwamba hata pale zinapokumbwa na changamoto kama vile vita, majanga ya asili na magonjwa ya miripuko sisi kama Watanzania na nchi nyingi za Afrika tumekuwa ndio wahanga wakubwa sana.
Tunateswa na matatizo ya wengine kwa sababu wao walishaamua kufanya kwa sehemu yao na kuanza uzalishaji wa mafuta ili kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo nchini kwao na hatimaye kuyatumia mataifa mengine kama soko lao, na kwa hilo wao waliweza na kufanikiwa lakini hata sisi nasi bado hatujachelewa kwani bado ukosefu wa nishati hiyo muhimu bado unalitesa taifa letu.
Jaribu kuwaza mpaka sasa vita vya Urusi na Ukraine vimepelekea kupanda kwa bei ya mafuta, vita vya Izraeli na Parestina navyo vimeathiri upatikanaji wa mafuta Tanzania lakini pia tukumbuke kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 jinsi ilivyopelekea kupanda kwa nishati ya mafuta na bidhaa nyingine tunazozitegemea kutoka nchi nyinginezo duniani, sisi hatujawahi kushindwa pale tunapoamua jambo, tunaweza kuamua kuwa na mafuta hayo ama nishati mbadala na kweli tukafanikiwa, tuliamua kuwa na bwawa kubwa lakuzalisha umeme na kweli tukafanikiwa na tuliamua kuwa na reli ya kisasa ya kutumia umeme tukaweza hata hili nalo tukiamua tunaweza kulimaliza na kubakia historia.
Mafuta yana umhimu mkubwa sana katika Taifa letu, pale kunapotokea mtikisiko wowote unaohusisha nishati hii ya mafuta hupelekea huduma nyinginezo nyingi kutikisika pia kwani biashara nyingi hutegemea nishati hii ya mafuta, kwani bidhaa zinazohusianishwa na biashara ni lazima zisafirishwe kutoka sehemu ya uzalishwaji hadi sehemu za walaji, jambo hili huhitaji mafuta, hivyo pale inapotokea changamoto yoyote kwenye upande huu wa nishati ya mafuta ndio hupelekea madhara kwenye sekta nyinginezo.
Tanzania ni nchi Tajiri sana hasa tunapozungumzia uwepo wa nishati mbalimbali yanayoweza kutumika kama mbadala wa nishati ya mafuta lakini pia hata tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa zimethibitisha uwepo wa mafuta katika sehemu ya bahari yetu ya hindi ambayo yakichimbwa yanaweza kuwa mwarubaini na suluhisho la tatizo la upatikanaji wa mafuta Tanzania.
Ili kukabiliana na tatizo hili la mafuta ni lazima tufanye mambo yafuatayo:-
1. Tuwekeze zaidi kwenye kufanya tafiti ili kuvumbua sehemu mbalimbali zenye mafuta ndani ya nchi yetu, Tanzania ni nchi kubwa yenye rasilimali nyingi sana duniani, rasilimali nyingine ni adimu hataduniani hazipatikani zaidi ya Tanzania tu, inawezekana tafiti zilifanyika na kuleta matokeo chanya lakini bado siyo maeneo yote, bado tunapaswa kufanya tafiti za kina ili kubaini zaidi sehemu ambazo tunaweza kupata nishati hiyo muhimu ya mafuta ili tuweze kuanza uzalishaji kwa haraka.
2. Kuhakikisha mafuta yanayogundulika kupatikana nchini kwetu yanachimbwa kwa gharama yeyote, na mafuta hayo yanaweza kuchimbwa na nchi yetu au kwa kushirikiana na wadau wengine hususani wawekezaji wa ndani au nje ya nchi yetu. Kufanyika kwa tafiti tu hakutoshi kama zinaishia kutoa majibu tu bila hatua za kuanza kufanyia kazi tafiti hizo, ni wakati wa kuhakikisha kila sehemu iliyogundulika kuwa na nishati hiyo ya mafuta serikali inaanza kufanya mchakato wa uchimbaji wa mafuta hayo.
3. Kuhakikisha nishati mbadala wa mafuta inazalishwa kwa wingi ili kuondokana na changamoto hii ya uhaba wa mafuta. Ni kweli kwamba athari za uhaba wamafuta zinajitokeza kwaukubwa kutokana na kwamba bado tunategemea nishati hii kwenye shughuli mbalimbali za maisha yetu bila kuwa na nishati nyingineya kutosha mbadala wa mafuta. Tanzania tumejaaliwa kuwa na uwepo wa gesi ya kutosha lakini haijatumika ipasavyo kuwa mbadala wa mafuta, magari ya watanzania wengi bado yanategemea mafuta abayo hayazalishwi kwetu badala ya kutumia gesi na nishati ya umeme ambayo kwa sasa tunazalisha kwa kiasi kikubwa.
4. Kupunguza kodi na tozo kwenye gesi au kuziondoa kabisa ili kuhakikisha gesi inashuka bei na watumiaji kuongezeka, hii pia itasaidia hata kwenye ulinzi wa mazingira. Kodi na tozo mbalimbali zikipunguzwa au kuondolewa kabisa kwenye gesi inayozalishwa hapa Tanzania itachochea watumiaji kuwa wengi na pia itawavutia watu kuitumia gesi hiyo kwenye vyombo vya usafiri badala ya mafuta na hayo yote yatachochewa na kushuka kwa bei ya gesi, inasikitisha mpaka sasa kunawatanzania ambao hawajawahi kuiona gesi wala kuitumia gesi hasa wale walioko vijijini, sababu kubwa ni bei ya raslimali hiyo kuwa juu bila shaka serikali ikiamua tunaweza kupiga hatua na kuhakikisha gesi inayozalishwa nchini kwetu tunaitumia kama mbadala wa mafuta.
5. Kupunguza bei ya mauzo ya unit za umeme ili kuhakikisha kila mtanzania anautumia umeme, kwani kutokana na uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali vilivyopo ndani ya nchi yetu unatosha kabisa kutumika kama mbadala wa nishati ya mafuta. Umeme wa kutosha unaweza kutumiwa kwenye vyombo vya moto kama mbadala wa mafuta kwa sababu kwa sasa kuna pikipiki zinazotumia nishati ya umeme,magari yanayotumia nishati ya umeme, hivyo tukitengeneza mazingira rafiki ya namna ya utumiaji wa nishati ya umeme hasa mara baada ya kuzalisha umeme mwingi kutoka katika Bwawa la mwalimu Nyerere ni wazi kwamba tunaweza kupambana na changamotohii ya uhaba wa nishati ya mafuta.
Hitimisho
Aidha ni mhimu kukumbuka kwamba kama taifa ni muhimu kuwa na maamzi ili kulinda maisha ya Watanzania ambao ndio walipa kodi, hivyo kuondoa kodi na tozo kwenye baadhi ya miundo mbinu au huduma hakupelekei kuikosesha nchi mapato bali kudumisha na kuboresha maisha ya watanzania ambao ndio walipa kodi.
Hivyo tukiamua kuyafanyia kazi yaliyotajwa katika andiko hili ni wazi kwamba tunaweza kupata suluhisho la changamoto za mafuta zinajitokeza mara kwa mara kutokana na mitikisiko inayoikumba dunia ikiwemo vita, magonjwa na majanga ya asili na hivyo kuipata Tanzania tuitakayo ndani ya miaka mitano au kumi ijayo.

Upvote
3