SoC02 Mwarobaini wa kutibu hali ya ubakwaji/kulawitiwa kwa watoto kwenye jamii yetu ya Watanzania

SoC02 Mwarobaini wa kutibu hali ya ubakwaji/kulawitiwa kwa watoto kwenye jamii yetu ya Watanzania

Stories of Change - 2022 Competition

kennymae

Member
Joined
Sep 13, 2022
Posts
6
Reaction score
2
MWALUBAINI WA KUTIBU HALI YA UBAKWAJI AU KULAWTIWA KWA WATOTO KATIKA JAMII YETU YA KITANZANIA.

Ubakaji maana yake ni ile ya mwanaume kumuingilia mwanamke bila ridhaa yake pasipo kujali ameingiliwa kwa kutumia kitu gani. Kulawitiwa ni ile hali ya mwanaume au mwanaume kuingilia kinyume na maumbile yake bila ridhaa yake.

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kupelekea watoto kubakwa/ kulawitiwa kwenye jamii zetu za kitanzania kwenye maeneo tofautitofauti nchini kwetu Tanazania.

Imani za kishirikina, Hili ni moja ya sababu kubwa sana inayochangia ubakaji na ulawiti kwa watoto.baadhi ya watu kwa kushirikiana na waganga wa kienyeji wanaaminisha kuwa ili uwe tajiri inabidi kufanyike tendo la ndoa na motto mdogo. Na hivyo kupelekea watoto wadogo kubakwa au kulawitiwa kisa tuu uyajiri na imani za kishirikina.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, Hii ni moja ya sababu ambayo watoto wanabakwa au kulawitiwa kwa kukosa mahala pa kujihifadhi na kukizi mahitaji yao kutokana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Matumizi ya dawa za kulevya mfano cocaine, heroin au bangi, Dawa za kulevya pia huchangia kwenye matukio ya ubakaji na ulawiti. Maana madawa ya kulevya humsababishia muhusika anayetumia kupoteza hali ya kuwa na huruma pamoja na uturivu wa akili.

Matatizo/Ugomvi baina ya familia moja na nyingine, hii ni ile hali ya mtoto anabakwa/ analawitiwa kwa lengo lakulipiza kisasi kwenye familia atokayo.

Matumizi ya pombe kali kupindukia ( Mfano gongo ), Ulevi wa pombe kali huchangia matukio ya ubakaji. Maana mtu anayetumia pombe kali huwa anapoteza hali ya ubinadamu na utu na hivyo kumpelekea mlevi kuwa na ujasiri wa kufanya tendo la ubakaji.

Ufahali wa kufanya ngono, Hii ni ile hali ya vijana kutaka kuonyesha ufahali wa kufanya ngono kwa vijana wenzao.

Shinikizo rika, Hali ya kikundi cha vijana wakiume kushauriana kufanya ngono na mwanamke mmoja kwa wakati mmoja.

Umaskini, hali ya kutokuwa na kipato cha fedha kwenye familia inaweza kupelekea mtoto kufanyiwa ubakaji/kulawitiwa kwa kuahidiwa kupatiwa.

Malezi anayopitia mbakaji akiwa mtoto (ugomvi wa wazazi, kufanyiwa ukatili ). Mifarakano ya wazazi au mtoto kufanyiwa unyanyasaji akiwa mdogo basi ni rahisi kuwa na chuki, hivyo kumfanya hatua yakupoteza utu na upendo na kuweza kufanya matendo ya ubakaji au kulawiti.

Majanga ya asili ( Mfano janga la njaa, mafuriko, ukame ). Kwa familia kukosa chakula kutona na majanga ya asili ni mazingira rafiki kwa mtoto kuangukia kwenye mazingira ya kubakwa, hususa kwa kudanganywa kupatiwa chakula au pesa yakununulia chakula.

Matatizo ya akili. Hali ya mwanaume au kijana wa kiume kuchanganyikiwa pia huweza kusababisha ubakaji/ulawiti maana hamu ya kufanya ngono ikimjia huwa siyo rahisi kuchagua mtu wa kufanya nae.
Pia maelezo yafuatayo hapo chini ni juu ya madhara/athari ya afya akili kwa watoto kutokana nakupitia tukio la kubakwa au kulawitiwa.

Kuwa na aibu au kupoteza hali ya kujiamini. Mtoto yoyote anayebakwa/ kulawitiwa hupatwa na aibu kutokana na hicho kitendo kufanyiwa na pia kumfanya kupoteza hali ya kujiamini.

Kujilaumu, Mara nyingi watoto wanaobakwa au kulawitiwa hupitia hali ya kujilaumu kwa nini hilo jambo amefanyiwa,ametendewa.

Kuwa na woga/hofu, Watoto wanaobakwa au kulawitiwa mara nyingi huwa wanakuwa na hofu au woga hususa wanapokutana au kumuona mtu aliyemfanyia tukio hilo la ubakaji/ulawiti.

Kuweweseka, Mara nyingi hupitia hali ya kuweweseka akiwa usingizini amelala au wakati mwingine hali hiyo humtokea anapomuona yule mtu aliyemfanyia tukio la ubakaji/ ulawiti.

Ndoto mbaya za usiku, hii ni moja ya madhara ambayo hupitia watoto waliobakwa/ kulawitiwa. Ni hali ambayo ni kujirudia kwa lile tukio la ubakaji/ kulawitiwa wakati akiwa amelala usingizini.( kuota ndoto ya tukio la kubakwa au kulawitiwa).

Hali ya kuwa na hasira, Mara zote watoto wanaopitia mateso ya ubakwaji/ ulawiti huwa na hasira hasa pale wamwonapo yule ambaye aliyemfanyia tukio la ubakaji/ulawiti.

Kupoteza tumaini na imani kwa jamii inayomzunguka. Mara nyingine mtoto aliyebakwa anaweza kupoteza hali ya kuwa na imani na matumaini na watu wanaomzunguka. Huwa anaamini kila mtu aliye mbele yake hana tofauti na yule aliyemfanyia tukio la ubakaji.

Hali ya kuwa na chuki, kutokana na hali ambayo mtoto aliyebakwa/ kulawitiwa hupitia humfanya kupoteza upendo na amani ya kuishi hivyo kumpelekea na kumtengenezea chuki kwa jamii inayomzunguka.

Kujutia kuzaliwa, hali hii huwatokea sana watoto waliyobakwa/ kulawitiwa. Watoto waliobakwa au kulawitiwa hupitia hali yakujutia kuzaliwa kutokana na kupitia maumivu yaliyotokana na kubakwa/kulawtiwa.

Kujitenga na watoto wenzake au jamii inayomzunguka, Watoto waliobakwa/ kulawitiwa hupitia hali hiyo kutokana na kupoteza imani, matumaini na upendo kwa jamii inayomzunguka pia na ile hali ya kuwa na hofu na woga huchangia watoto kujitenga.

Kuwa na msongo wa mawazo, hii ni moja ya madhara watoto ambayo hupitia watoto waliobakwa/ kulawitiwa. Hivyo watoto waliopitia hiyo hali hupitia hali ya kuwa na mawazo kupita kiasi yaliyochangiwa na tukio la ubakaji/ kulawitiwa.

Kukata tama ya kuishi, hii ni moja ya madhara ambayo watoto waliobakwa au kulawitiwa hupitia. Kutokana na hali ya msongo wa mawazo kupita kiasi yaliyosababishwa na tukio la ubakaji/ kulawitiwa na kupelekea kupoteza hamu na hali ya kuishi.

kutamani kujiua, hii ni moja ya madhara ambayo hupitia watoto wanaobakwa/ kulawtiwa. Watoto wanaobakwa au kulawitiwa hupitia changamoto ya kuhitaji kujiua kutokana na hali ya kukata tamaa ya kuishi yaliyochangiwa na msongo wa mawazo kupindukia.

Maelezo yote hayo juu ni kutaka kutoa elimu juu ya sababu zinazoweza kupelekea ubakaji/ uulawiti kwa watoto kwenye jamii zetu ndani ya nchi yetu pendwa Tanzania, na pia juu ya kuelimisha madhara ya afya ya akili wanayoweza kuyapata watoto waliobakwa au kulawitiwa na mtu au watu wanaomzunguka katika jamii zetu za kitanzania.

Pia kama jamii zetu zitapata elimu na uelewa juu maelezo ya sababu na madhara ya kubakwa au kulawitiwa kwa watoto, ni imani yangu kuwa hiyo ndiyo tiba/ mwalubaini wa kupunguza matukio hayo kwa kiasi kikubwa na mwishowe kuisha kabisa.

Imeandaliwa na KENNY EDWIN
 
Upvote 4
Habari yako ndugu.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, kuipigia kura yako na kuchangia mawazo au mapendekezo juu ya nakala inayohusu Afya zetu Watanzania:-


Ahsante!!
Kwanza joggers, ni makala nzuri inayoelemisha na kutoa suluhu. Ila mm nafikiria hivyo vifupisho vya kiingereza vitakupunguzia alama kwamajaji wenye asilmia 70.
Ila kura yangu umeipata🤝.
 
Mwanaume naye anaweza kubakwa na sio mwanamke tu, mwanamke naye anaweza kulawitiwa na sio mwanaume tu
 
Kwa hiyo umesema UBAKAJI ni kitendo cha mwanaume kumuingilia mwanamke bila idhini yake na sio UBAKAJI ni kitendo cha MTU kumuingilia MTU bila idhini,umekosea hapo kuweka mwanaume kwani hujawahi sikia Jinsia KE kubaka Jinsia ya ME?
 
Back
Top Bottom