nyamwingi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 944
- 872
Ni msiba mkubwa kwa Familia yake maana siku 12 zilizopita amefariki mtoto wake wa kiume ,ambaye pia alisemekana sana kuwa ni kipenzi chake.Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga
Mzee Moyo ambaye pia ni Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano #Zanzibar
Inna lillah wainna ilayhi rajiuna.
======
Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na chama cha Mapinduzi akiwa na kadi namba 7.
Mzee Moyo ndiye alikuwa Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Mzee Hassan Nassor Moyo alivuliwa uanachama wa chama cha mapinduzi CCM, hatua iliyofikiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja viswani Zanzibar
Mada mbalimbali zinazomhusu Mzee Moyo
- Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM
- CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo
- RAI: MASWALI na MAJIBU; HASSAN Nassor Moyo: Sio rahisi kuuvunja Muungano huu
Allah awape subra familià ya mzee Hassan Nasoro Moyo.