TANZIA Mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo afariki dunia

Ni msiba mkubwa kwa Familia yake maana siku 12 zilizopita amefariki mtoto wake wa kiume ,ambaye pia alisemekana sana kuwa ni kipenzi chake.
Allah awape subra familià ya mzee Hassan Nasoro Moyo.
 
Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga
Duh...!.
Huyu ndiye shuhuda pekee wa kusainiwa muungano wetu adhimu, aliyebaki kuwa hai.
Kifo hiki maana yake mashuhuda wote wa kusainiwa kwa The Articles of The Union Between Tanganyika and Zanzibar, wametangulia mbele ya haki.
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?
RIP Mzee Hassan Nassor Moyo.
Inna lillah wainna ilayhi rajiuna

P
 
RIP! Naomba kuuliza , kwake ni Tanga, halafu akwa mwasisi wa siasa za Zanzibar, kwa vipi?
Mbona Hussein mwinyi kwako ni ukerewa lkn kapitishwa Dodoma aje agombanie urais Zanzibar kwahiyo Tanganyika ndio wanavo itawala zanzibar
 
Serikali nyingi za Afrika zingekuwa na utaratibu wa kusikia 'Mawazo' na 'Changamoto' za 'Critics' mbalimbali huenda Bara hili 'lingefanikiwa' zaidi tu.
Serikali yetu inasikia hizo changamoto, mpaka sasa inaitwa "serikali sikivu"
 
Huwa mnakasi ya kipanga kupost nyuzi sijui kwa sababu gani tu!

Picha ina sura mbili, sasa nani ndiyo nani?

Ukiamua kuhabarisha umma, jitahidi kudhibiti maswali yanayojengwa juu ya maswali kwa kuifafanua mada na kuweka wasifu wa mhusika.

Acha hizo hata kama umeamka vibaya. Mzee picha inaonesha dhahiri ni nani hapo. Huyo nzee mwingine nywele kapaka black ni kijana.
Mzee Moyo kaumaliza mwendo, apumzike kwa amani. Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
 
Mbona Hussein mwinyi kwako ni ukerewa lkn kapitishwa Dodoma aje agombanie urais Zanzibar kwahiyo Tanganyika ndio wanavo itawala zanzibar
Ok, wenzako wanasema huku ni kwa kuishi tu! nakubaliana nao kabisa
 
Poleni ndugu,jamaa na marafiki.
 
Poleni wafiwa. Hata Shein naye akimaliza kutawala Zanzibar atarudi nyumbani kwake bara. Na sasa Hussein Mwinyi anatafuta kutawala Visiwani, akimaliza arudi nyumbani kwake bara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…