Mkuu japo sio dhamira kuu ya huu uzi naomba nikupe elimu ya uendeshaji wa kampuni kwa Tanzania na takwa la sheria lilivyo. Itakusaidia wewe pamoja na wengine pia.
Kwanza kabisa Mkuu nitaanza na maelezo yako mwenyewe hapo juu.
Kama ni kampuni iliyosajiliwa Brela ni wazi mpo zaidi ya mtu mmoja yaani wamiliki hapo mpo wawili au zaidi.
Sasa hao wawili au zaidi ndio wamiliki na kimsingi ndio wawekezaji, ikiwa mna mtu mwingine nje ya nyie ambaye kaweka fedha yake hapo mmeenda nje ya sheria za uendeshaji wa makampuni Mkuu (rekebisheni hilo, nitawaeleza kivipi).
Sasa hapa umesema unatafuta mwekezaji japo ulishasema kuna mwekezaji (sio kesi).
Yeyote atakayeingia kama mwekezaji hapo ni lazima awe sehemu ya wamiliki wa hiyo kampuni ili muende sawa, sasa ninyi nmachotaka ni fedha za uendeshaji labda na utendaji hapo mtamhitaji mtu ambaye atakuwa mwanahisa wa mtaji huyu atatoa fedha tu na kusubiri mgao wa faida baadae.
Sasa mgao wa faida mtaupataje?, nimeona umesema mtakubaliana ila kimsingi ni rahisi sana sababu faida itatoka kwa uwiano wa asilimia za umiliki wa hiyo kampuni yenu ambao utaupata kwenye idadi.za hisa kwa kila mwanahisa.
Jambo lingine muhimu sana ni kuzingatia sheria ya makampuni maana kuna uwezekano mkubwa hata mmoja wenu hamjawahi kununua hisa alizochukua kwenye hiyo kampuni.
Pili leseni za mamlaka husika za shughuli mnazozifanya, kodi na mengineyo.
Haya yote akija mtu ambaye kweli amelenga kuwekeza kwenu atatafuta wakili akija kwetu mawakili tutaanza na hayo kwenye kampuni yenu yakiwa magumashi tutaishia kumshauri tofauti na mataraji yenu Mkuu.
Hivyo zingatia hayo kwanza Mkuu, ila pia kama unatafuta mtu serious na upo serious ungeweka details kadhaa za kawaida hapa Mkuu mfano jina la kampuni, namba ya usajili na standard search report kutoka Brela.
Ukiwa na swali lolote usisite kuuliza Mkuu.
Karibu na kila la kheri.