The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mwekezaji wa Kitanzania, Josiah Mrimi, ameweka wazi changamoto alizokumbana nazo wakati wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi, Murikado Food Supply, kilichopo katika kijiji cha Itulahumba, wilaya ya Wanging'ombe, mkoa wa Njombe.
Akizungumza siku ya Jumatatu mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Mrimi amesema ingawa amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kutoa ajira kwa zaidi ya watu 500, bado anakabiliwa na changamoto za miundombinu ya barabara.
Hata hivyo, ameshukuru msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kwa kusaidia upatikanaji wa umeme, ambao umekuwa msaada mkubwa kwa uendeshaji wa kiwanda hicho baada ya kutoa maagizo na kusimamia uwezeshaji wa miundombinu hiyo.
Mrimi amesema ujenzi wa kiwanda hicho, uliogharimu zaidi ya TSh bilioni 5, haukuwa mwepesi kwani alikumbana na vikwazo kadhaa, ikiwemo baadhi ya watu waliotaka kukwamisha juhudi zake. Amesema hapo awali, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walidai TSh milioni 800 ili kumruhusu kupitisha barabara ya kufikia eneo la uwekezaji wake.
Kwa upande wake, Waziri Prof. Kitila Mkumbo ameagiza wataalamu, wakiwemo wa TARURA, kuhakikisha wanabadilika na kuweka mipango madhubuti ya ujenzi wa barabara zinazounganisha maeneo ya shughuli za kiuchumi, ili kusaidia uwekezaji na maendeleo ya sekta ya viwanda.