Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Dewji (MO), amewaonesha Wapenzi na Mashabiki wa Simba ramani mpya ya Mo Simba Arena akisema huo ni mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio ya Club hiyo baadaye.
Akiongea leo October 06,2024 kwenye Mkutano Mkuu wa Club hiyo, Mo Dewji amesema "Hii ni ramani mpya ya Mo Simba Arena, mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio yetu baadae, tunatarajia kujenga kambi bora ya mazoezi itakuwa na gym, majengo ya malazi, kituo cha lishe, bwala la kuogolea, kituo cha burudani, viwanja vitano vya kisasa zaidi ya hayo kujenga makumbusho ya klabu na kuanzisha chuo cha maendeleo ya Vijana ili kulea vipaji vya soka Nchini"
"Ili kufanikisha yote haya tunasubiri mchakato wa mabadiliko ya Simba kukamilika, tuko katika hatua za mwisho, ujenzi wa miundombinu hii unakuja na gharama kubwa, ni ngumu kuanza huu ujenzi bila mfumo kubadilika"
Pia, Soma:
• PICHA: MO Dewji na Mangungu washikana mikono kwa mara ya kwanza
• Hotuba ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Simba SC Mo Dewji kwenye mkutano mkuu wa Club 2024