Mwelekeo mpya bungeni, Pinda atoa hoja kutuliza hali ya hewa

Mwelekeo mpya bungeni, Pinda atoa hoja kutuliza hali ya hewa

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanikiwa kutuliza hali ya hewa bungeni baada ya kutoa mapendekezo yaliyoungwa mkono na pande zote zilizokuwa zinavutana kuhusu kupitisha baadhi ya vifungu vya Kanuni za Bunge la Katiba.

Katika mapendekezo yake yaliyoungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Pinda alisema: “Nataka kuwaomba wenzangu wote kwenye maeneo hayo (yenye malumbano) tukiwa tunayapitia kama hatutaelewana tuyaache kwa muda na kumwomba Mwenyekiti aunde timu ya watu wazima na wenye busara wajaribu kuyatazama. “Tujadiliane, tushindane kwa lugha za staha, tusitumie lugha inayoweza kukasirisha. Isiwe mimi nimesema, mimi nimesema...”

Waziri Mkuu, aliwataka wajumbe wajiepushe na lugha za kuudhi ambazo zinaweza kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya.

Pinda alilazimika kuingilia kati baada ya kutokea mgawanyiko mkubwa wa namna ya kupiga kura kupitisha vifungu vya rasimu.

Akiunga mkono ushauri huo, Mbowe alisema Bunge limejaa hisia za hofu ndani na nje, jambo ambalo linatia wasiwasi wa kupatikana kwa Katiba Mpya. Alisema iwapo wajumbe watashirikiana na kuweka kando masilahi ya vyama, idadi yao katika makundi, Katiba inaweza kupatikana.

Vuai alionya kuhusu matumizi ya lugha za kuudhi huku Profesa Lipumba akiwataka wajumbe kuzingatia masilahi ya Taifa kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete na kutengeneza Katiba ya Watanzania wote bila ya kujali masilahi binafsi.

Upigaji kura bungeni vita

Awali, mjadala wa utaratibu wa upigaji kura katika Bunge hilo ulichukua sura mpya baada ya kudaiwa kuwapo ushawishi unaohusisha utoaji wa bahasha ili kutaka kuungwa mkono katika misimamo inayokinzana.

Habari zilizopatikana zilidai kuwa watuhumiwa katika sakata hilo ni baadhi ya wajumbe ambao ni mawaziri na mbunge mmoja wa CCM. Vigogo hao wanadaiwa kuwashawishi wajumbe ambao hawatokani na vyama vya siasa ili kupitisha agenda ya kura ya wazi kirahisi.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mjumbe wa Bunge hilo, Julius Mtatiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, alisema: “Jaribio la kuzuia kura ya siri limechukua njia za aibu, baada ya CCM kutumia fedha kushawishi wajumbe.”

Katika ujumbe huo ambao alikiri kuuandika, Mtatiro aliwataja wajumbe watatu ambao ni mawaziri kuwa waliwakaribisha wajumbe kwenye makazi yao na “kuwaandalia chakula cha kutosha, vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine, huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao hivyo vya siri.” Mmoja wa waliotajwa ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe aliyedaiwa kuwaalika wawakilishi wa wafugaji na kuwapa chakuka na bahasha.

Akijibu tuhuma hizo, pamoja na kukiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe na kula nao chakula, alikana tuhuma za kuwahonga ili waunge mkono msimamo wa chama hicho. Alisema Mtatiro amemdhalilisha, hivyo anawasiliana na mwanasheria wake ili kumfikisha mahakamani.
 
Katika ujumbe huo ambao alikiri kuuandika, Mtatiro aliwataja wajumbe watatu ambao ni mawaziri kuwa waliwakaribisha wajumbe kwenye makazi yao na "kuwaandalia chakula cha kutosha, vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine, huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao hivyo vya siri." Mmoja wa waliotajwa ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe aliyedaiwa kuwaalika wawakilishi wa wafugaji na kuwapa chakuka na bahasha.

Akijibu tuhuma hizo, pamoja na kukiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe na kula nao chakula, alikana tuhuma za kuwahonga ili waunge mkono msimamo wa chama hicho. Alisema Mtatiro amemdhalilisha, hivyo anawasiliana na mwanasheria wake ili kumfikisha mahakamani.

Sasa kama wote wanapewa POSHO sawa kwa nini awaalike wajumbe wengine kwenye chakula?Kwa nini awalipie?Haingii akilini hiyo pia ni rushwa tosha.
 
Pinda angelianza kwanza kuwakemea CCm wenzake kwa waraka ule wa siri, otherwise ni unafiki tu kama kawaida yake.
 
Pinda angelianza kwanza kuwakemea CCm wenzake kwa waraka ule wa siri, otherwise ni unafiki tu kama kawaida yake.

mkuu, huwezi kuzuia chama cha siasa kuwa na mkakati katika suala kama hili. By the way ccm ndo chama tawala hivyo huwezi kukwepa
 
Hivi kwenye bunge la katiba vyeo vinatumika au huwa vinawekwa pembeni?? What I am asking is ............. Je Waziri Mkuu anatambulika kama Waziri Mkuu anapokuwa kwenye bunge la katiba!!??
 
Sasa kama wote wanapewa POSHO sawa kwa nini awaalike wajumbe wengine kwenye chakula?Kwa nini awalipie?Haingii akilini hiyo pia ni rushwa tosha.

utaratibu wa kualikana kwenye chakula upo miaka yote. Haujawahi kulalamikiwa na hii ni katika kudumisha utamaduni wetu wa ukarimu
 
Kwa hali iliyo sasa, bungeni kunahitajika busara ya hali ya juu sana! Wajumbe watambue kuwa katiba inayotungwa ni ya taifa, na sio ya chama au kundi lolote lile!
 
Hivi kwenye bunge la katiba vyeo vinatumika au huwa vinawekwa pembeni?? What I am asking is ............. Je Waziri Mkuu anatambulika kama Waziri Mkuu anapokuwa kwenye bunge la katiba!!??

kwani wewe ulitaka atambulike vipi? Je baba yako anapoenda kuhudhuria mkutano wa wazazi anaendelea kuwa baba yako au ni mzazi tu kama mzazi mwingine?
 
Kwa hali iliyo sasa, bungeni kunahitajika busara ya hali ya juu sana! Wajumbe watambue kuwa katiba inayotungwa ni ya taifa, na sio ya chama au kundi lolote lile!

hakika mkuu. Na ndo maana mwenye busara kuliko wote, Pinda akaitwa kutuliza hali na ndo maana hata Lipumba ambaye asubuhi ya jana alikuwa kama mlevi, jioni aliongea maneno ya hekima
 
utaratibu wa kualikana kwenye chakula upo miaka yote. Haujawahi kulalamikiwa na hii ni katika kudumisha utamaduni wetu wa ukarimu

Kaka kwa sakata lilokuwepo hasa kwa chama tawala kutaka kuhodhi bunge hilo asingejitia kitanzi kwa kuwaalika wajumbe wengine toka taasisi nyingine,na inawezekana hali zao kiuchumi si nzuri sana kama yeye.Amefanya kosa akiri kosa alilolifanya.Kwa msuguano uliokuwepo si vyema kutoa TAKRIMA kwa wajumbe,mie nitaiita RUSHWA tu kwa wajumbe ili wafuate matakwa ya aliyewateua.Ukiwa MZALENDO utafikiria nje ya boksi.
 
Nakumbuka katika ile orodha ya Nape ya mawaziri MIZIGO, Prof. Magembe alikuwepo. Sasa huu mzigo unataka kutuharibia mchakato wa upatikanaji wa KATIBA.
 
Kaka kwa sakata lilokuwepo hasa kwa chama tawala kutaka kuhodhi bunge hilo asingejitia kitanzi kwa kuwaalika wajumbe wengine toka taasisi nyingine,na inawezekana hali zao kiuchumi si nzuri sana kama yeye.Amefanya kosa akiri kosa alilolifanya.Kwa msuguano uliokuwepo si vyema kutoa TAKRIMA kwa wajumbe,mie nitaiita RUSHWA tu kwa wajumbe ili wafuate matakwa ya aliyewateua.Ukiwa MZALENDO utafikiria nje ya boksi.

dada, kwani mie kama nakutaka halafu nikakujengea nyumba, nikakununulia gari na kila unachohitaji nakupatia hata kabla ya kukutamkia kuwa nakupenda au wewe huna mapenzi na mie, mwisho wa siku ukanikataa kwa kutumia utashi wako hapo mie nitakulaumu kwa lipi? Hata kama hao wajumbe wamealikwa kwenye dinner haina maana kuwa ndo wanashurutishwa kwenye maamuzi. Hata Mbowe pia katoa dinner kwa wawakilishi wa NGO
 
hakika mkuu. Na ndo maana mwenye busara kuliko wote, Pinda akaitwa kutuliza hali na ndo maana hata Lipumba ambaye asubuhi ya jana alikuwa kama mlevi, jioni aliongea maneno ya hekima
sikubaliana na dhana yako kuwa pale bungeni mwenye busara kuliko wote ni pinda, hapana, kuna watu wengi tu, kama kina sitta, maprof na kadhalika. Pinda aliwakilisha tu upande wa serikali!
 
kwani wewe ulitaka atambulike vipi? Je baba yako anapoenda kuhudhuria mkutano wa wazazi anaendelea kuwa baba yako au ni mzazi tu kama mzazi mwingine?

naona uko shift ya asubuhi leo. au mnakuwa assigned per thread?!
 
naona uko shift ya asubuhi leo. au mnakuwa assigned per thread?!

kwani mtu kujitokeza jukwaani na kuwaambia ukweli watanzania ndo kusema kuwa umekabidhiwa majukumu hayo? Haya, na wewe nani kakutuma kuja kuleta upuuzi humu? Kumbuka uzuri wa JF ni kuwa na active members. Si kama kule kwingine
 
sikubaliana na dhana yako kuwa pale bungeni mwenye busara kuliko wote ni pinda, hapana, kuna watu wengi tu, kama kina sitta, maprof na kadhalika. Pinda aliwakilisha tu upande wa serikali!

Mkuu, inaonekana unaongea tu kwa hisia na hujui ukweli. Kumbuka,busara ya mtu haipimwi kwa kumwangalia au kiwango cha elimu yake au umri wake
 
dada, kwani mie kama nakutaka halafu nikakujengea nyumba, nikakununulia gari na kila unachohitaji nakupatia hata kabla ya kukutamkia kuwa nakupenda au wewe huna mapenzi na mie, mwisho wa siku ukanikataa kwa kutumia utashi wako hapo mie nitakulaumu kwa lipi? Hata kama hao wajumbe wamealikwa kwenye dinner haina maana kuwa ndo wanashurutishwa kwenye maamuzi. Hata Mbowe pia katoa dinner kwa wawakilishi wa NGO

Siwezi kuunga mkono kwa sababu tu Mbowe amefanya pia.Yote ni rushwa.Utashi unaouongelea watanzania hatuna.Ingekuwa nchi nyingine kama Kenya ningeweza kusema watakuwa na uwezo wa kuthubutu vinginevyo bado ni rushwa tu.Kwa utashi tu hata kama haujanunua hilo gari au nyumba natakiwa kukupa msimamo wangu na kama utafantya ulivyoamua basi ni utashi wako sababu utakuwa unaelewa fika uamuzi wangu.Kwa kusema HAPANA baada ya kupewa vyote sijui kama nitakuwa nimeitendea haki nafsi yangu na yako.SO ni vizuri kuwa na msimamo kabal ya matokeo hasi au chanya.
 
Back
Top Bottom