Mweleweshe hii mtu yeyote ni muhimu sana

amigooo

Senior Member
Joined
Jun 30, 2012
Posts
115
Reaction score
18
Calcium ni madini muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno, vidonge vine hutoa asilimia 100 ya kiasi cha calcium itakiwayo kwa siku katika mwili ina 1000mg ya calcium pamoja n 400iu ya vitamin D na 400mg za Magnesium nyongeza ya bidhaa hizo mbili za mwisho ni muhimu kusaidia uwezo wa juu wa unyonywaji wa calcium mwilini. Bidhaa hii ni muhimu na itumike wakati wa kula chakula ili iweze kuingia mwilini. Damu ikikosa bidhaa hii huiamuru parathyroid hormone ichukue kwenye mifupa na meno na kusababisha mifupa kuwa dhaifu na rahisi kuvunjika(osteoporosis)
Pia wajawazito huwa calcium nyingi hutumika kwa ajili ya mtoto aliye tumboni.

INASAIDIA: Kuimarisha mifupa, meno, mapigo ya moyo, misuli, ugandaji wa damu na hormones kufanya kazi vizuri.
 

Attachments

  • calcium.jpg
    8 KB · Views: 366
Umeandika kama sisi wote ni wataalamu kama wewe, binafsi nimeshindwa kuelewa sijui itakuaje nikitaka kumuelewesha mtu
 
Sasa ndugu, vidonge vikitoa 100% ya calcium inayohitajika mwilini ina maana calcium tunayopata kwenye chumvi, dagaa na vyakula vingine ndo itakuwa excess? Si tutajipatia magonjwa sasa ya ziada?

Mie huwa najiuliza haya mavidonge mnayotuambia tutumie sijui omega 3, calcium, vile vya vitunguu swaumu na mengineyo. Kama tukiwaendekeza, asubuhi ukiamka unatenga sahani ya dawa kabisa unakunywa vidonge 40? Manake calcium tu ni vidonge 4! Mngetengeneza perfume zao na lipstic tuwe tunajipodolea asubuhi yaishe.
 

teh teh teh, kweli Mtambuzi na Mama Ngina mtoto mnae
 
Last edited by a moderator:


Calcium inapatikana kutokana na baadhi ya vyakula lakini ni wangapi wana uelewa mzuri na pia vyakula tunavyokula vinakuwa vimeandaliwa katika mazingira gani.
 

Hapa sina mtoto haki ya mama........
Binti umepinda mdomo kwa kuzodoa watu.... mweh!
 
Mwanangu amigoo, sijui hata kama wewe unalielewa hilo jambo unalotaka mimi nielewe. Maana ya hoja yangu ni kwamba there is nothing so special to deserve such attention in the first place. Nadhani sasa umeelewa.
 
Sio kuzodoa banaa. Siku hizi usikae kunywa thupu bar, wamasai wanakuja na dawa za kuongeza nguvu za kike, mara washosti wanauza forever, sijui edmark! Sasa home si kutageuka phamacy?
Hapa sina mtoto haki ya mama........
Binti umepinda mdomo kwa kuzodoa watu.... mweh!
 
Sasa si kuna alternative lishe ndugu? Badala ya kutupa lishe kwa vidonge 4 kwa siku, ungetuambia tule ugali na dagaa wa nazi na spinach paraboiled. Tungejichana na kufurahia afya njema. Wasiwasi wangu ni vidonge kutoa lishe ya siku (daily allowable.intake)
Mimi sizungumzii dawa bali nazungumzia lishe wadau
 
Hauwezi kureplace 100% ya lishe kwa vidonge.
Calcium inapatikana kutokana na baadhi ya vyakula lakini ni wangapi wana uelewa mzuri na pia vyakula tunavyokula vinakuwa vimeandaliwa katika mazingira gani.
 
Hauwezi kureplace 100% ya lishe kwa vidonge.

Ndo hapo sasa badala ya kununua hivyo vidonge si bora ninunue vyakula vyenye calcium! Mzizimkavu njoo bwana na vyakula vya kuongeza calcium umekaa kimya muda mrefu ona tunaletewa mbadala wa vyakula nadhani baada ya kujua vyakula vyenye calcium naweza elimisha watu wakanielewa
 

I wonder, ishu simpo kabisa.. Angeanzisha sredi yenye orodha ya vyakula ambavyo vina madini ya Calcium, au angekuwa straight kuwa anauza vidonge, siyo kutupa darasa eti tukawafundishe na wenzetu kana kwamba tumemwelewa.
 
mimi sizungumzii dawa bali nazungumzia lishe wadau

acha janjajanja yako banaaa..

Wee huoni tangazo lako la vidonge vya foreverliving?...au ulikuwa unajuwa umetuwekea sahani ya wali samaki na matunda kibaooo plus mboga za majani na glass ya maziwa????

haya kama unatangaza lishe wapi ushawahi kusikia hoteli menu inavidonge vinne vya calcium na magnesium ulizoandika hapo???

ushakuwa acha utoto..na hili ni tangazo dogo la biashara tafuta pahala pake upeleke huku ni kwa watu wenye uhitaji wa kitabibu/ madaktari.
 
Siyo kuwa watu hawali chakula bali wanakula lakini hawana uelewa mzuri wa vyakula. Mfano huo ugali wengi wanakula sembe jambo ni dogo sana kulielewa kuwa siyo sahihi. Vyakula tunavyokula vingi havina vile viasilia vinavyohitajika mwilini sbb ya madhara mengi yatokanayo na uharibifu wa mazingira pia.
 
Hauwezi kureplace 100% ya lishe kwa vidonge.

Vidonge siyo kuwa inaanisha ndiyo dawa. Naona hapo ndiyo panapokuletea tabu. Hiyo ni lishe ambayo imetolewa katika mfumo wa tembe tu. Mtu anaweza akala sahani ya chakula na asipate hata 1/16 ya kinachotakiwa mwilini.
 
Umeeleza vizuri ila umekuja kuaribu kwenye hyo picha!! Promo Only.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…