Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
MWEMBAMBA AKUTANA NA ZAKAYO MTOZA USHURU.,
Ndugu yangu mwembamba nikupe siri kali, ukiwa mkubwa usifanye kama ngosha kuwasumbua sumbua "wanene" wanaokuweka mjini. Ukiwasumbua "wanene" kuwadai kodi ni sawa na kumkumbatia papa nyangumi ndani ya maji halafu utake kumuua,atakuua wewe.
Ukiwa mkubwa au ukibahatika kuwa "Zakayo mtoza ushuru" ndugu yangu "draw the line" sema kabisa "ninyi wanene sitawagusa, sasa hivi zamu yenu ya kula asali, sasa hivi zamu ya wembamba kutozwa tozo.
Ukiwa mkubwa waambie wanene wakishauza dhahabu,au wakishashusha mzigo bandarini wapitie kwenye nyumba yako kubwa mnywe mvinyo kidogo kuliponya tumbo, na kuumwagilia moyo, yashike nikwambiayo ndugu yangu.