Mwenda: Waandishi andikeni makubwa yaliyofanywa na wanawake nchini

Mwenda: Waandishi andikeni makubwa yaliyofanywa na wanawake nchini

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Suleiman Mwenda amewaomba Waandishi wa historia kuendelea kuenzi na kuthamini mchango uliotolewa na wanawake kabla na baada ya Tanzania kupata uhuru.

Mhe. Mwenda ametoa ombi hilo Jana Jumanne Machi 08, 2022 wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya Shule ya Wasichana Tumaini mjini hapa.

“Ni bahati mbaya sana kutotaja mchango mkubwa uliofanywa na Mwana mama shupavu kabla na baada ya uhuru
wa Taifa letu Hadija Kamba ambaye aliwahi kusema na kudai kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo
endelevu.” Alisema Mwenda.

Aidha, aliongeza kuwa kauli mbiu hii “Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu” ambayo leo tunajivunia ni kauli ya kishupavu na ukomavu iliyosemwa na Mwana Mama Hadija Kamba ambaye ni mmoja wa waasisi wa Taifa la Tanzania na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinaongoza nchi yetu.

Kwa mara ya kwanza Hadija Kamba alisikika akitajwa mwaka 1985 na Mwalimu Julius K. Nyerere wakati akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika ukumbi wa Diamond Jubilee akiwa anawaaga na kuwatangazia rasmi kuwa anang'atuka katika nafasi ya urais na kubaki kuwa Mwenyekiti wa CCM.

Mwalimu Nyerere alisema kuwa katika miaka 24 ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna Mwanamama ambaye alikuwa akimshangaza kwa sababu ni Mwanamama ambaye alipambana enzi za ukoloni ili kulipatia Taifa Uhuru.

“Katika kina Mama waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano enzi za ukoloni katika siku ngumu na hatari ni Khadija Komba." Alisema Mhe. Mwenda.

Baada ya kupata uhuru Mwalimu Nyerere alimwita Hadija Kamba nakutaka kumpa cheo ingawa alikataa na kuyasema maneno ya kishujaa ambayo leo sie tunajivunia.

"Lengo la kushiriki na kuingia katika mapambano ya kuondoa ukoloni ilikuwa ni kuhakikisha tunapata jamii ya haki na usawa, hivyo nimeridhika kabisa kwa sababu lengo langu limetimia kwa sababu sasa Waafrika wanathaminiwa katika nchi zao na
hawatawaliwi tena.” Alisema Kamba. Kauli hiyo ilimfanya Mwalimu Nyerere kusema kuwa sio watu wengi walioshiriki mapambano hayo na hawakuwa wanalenga kupata madaraka isipokuwa ni wa chache akiwemo Hadija Kamba.

“Kwa bahati mbaya sana historia yetu kipindi cha ukoloni, mapambano dhidi ya ukoloni na hata katika kupata uhuru wetu hawatajwi sana wanawake hawa muhimu walioshiriki kwa namna moja au nyinginge kuhakikisha tunapata uhuru wetu.” Alikumbusha Mhe. Mwenda na kuongeza kuwa historia yetu imetaja sana wanaume kama vile wakati wanaume wakipambana hawakuwa na akina Mama hawa, hivyo ni wakati sasa kwa Waandishi wetu kuenzi na kuthamini michango iliyofanywa na wanawake hawa katika kulijenga Taifa letu” Alisisitiza Mhe. Mwenda.

IMG-20220309-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom