Mwendelezo vituko IFM Mwanza Campus, TV yawashwa chumba cha mtihani

Mwendelezo vituko IFM Mwanza Campus, TV yawashwa chumba cha mtihani

Mbwa kala mbwaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
218
Reaction score
389
Hii kampasi majanga yanazidi kuongezeka na wahusika msipo chukua hatua hamtutendei haki wanafunzi.

Leo jumapili sisi wanafunzi wa BIRM 3 tukiwa tunafanya mtihani wa strategic management lecture 7, tukiwa dakika za mwishoni ghafla aliingia mfanyakazi wa computer lab Mr Swai huku kashika remote mkononi. Moja kwa moja akaenda mbele na kuwasha desktop ya kufundishia. Lahaula, si akawasha na projector na kurusha matangazo ya kombe la dunia kwa sauti kubwa ukutani huku mtihani unaendelea!

Tumejiuliza maswali mengi juu ya aina ya wafanyakaz wanao ajiriwa hapa Mwanza Campus. Haya Ni maajabu ambayo hata katika mitihani ya chekechea huwezi kuyaona. Huyu ndugu ni kichaa?? Maana wasimamizi wa mtihani ilibid watumie nguvu ya ziada kumdhibiti na kuzima matangazo Yale yasilete bighudha.

Hebu mamlaka za IFM angalieni sampuli ya baadhi ya wafanyakaz wenu hapa Mwanza Campus, wanatia aibu na kinyaa.

Pathetic!

Soma pia:

Mtoa post una shida sasa mambo madogo kama hayo unafanya mada ya watu kujadili inaonekana uwezo wako wa kufanya decision making n mdogo sana, unakosa Leadership skills nashangaa hata hilo somo limeshindwa kukubadilisha kifikra
Unaona Jambo dogo hili
 
HAWA MADOGO WANATIAA AIBU SANA HUMU NDANI
 
Mtoa post una shida sasa mambo madogo kama hayo unafanya mada ya watu kujadili inaonekana uwezo wako wa kufanya decision making n mdogo sana, unakosa Leadership skills nashangaa hata hilo somo limeshindwa kukubadilisha kifikra
Wewe ndio una shida mkuu, unashindwa kuchata namna gani jambo linatakiwa kufanyika kwa usahihi na kwa wakati upi katika kazingira yapi.
 
Hayo mambo si myamalize hapo chuo habari ya upande mmoja unataka kututoa chambo
Hapa ndipo mahala sahihi kuibua mambo ya ajabu kama haya, kama ulikua hujui, forum hii inafuatiliwa na watu wengi mnoo, na imekua msaada mkubwa katika kuibua changamoto ndogo ndogo na kubwa pia.
 
Hapa ndipo mahala sahihi kuibua mambo ya ajabu kama haya, kama ulikua hujui, forum hii inafuatiliwa na watu wengi mnoo, na imekua msaada mkubwa katika kuibua changamoto ndogo ndogo na kubwa pia.
Vitu vingine ni Very minor
 
Back
Top Bottom