babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,222
- 3,173
Aliyekuwa mwendeshaji wa kipindi maarufu Uingereza cha Love Island, Caroline Flack amejiua jana nyumbani kwake London.
Caroline alikuwa ni mwendeshaji wa kipindi hicho kwa miaka kadhaa mpaka mwisho mwa mwaka Jana ambapo alilazimika ku resign kutoka na tuhuma za kumpiga mpenzi wa kiume na taa ya mezani.
Caroline alikuwa pia ni mshindi wa Strictly come dancing 2014 na mtangazaji wa Xtra Factor kabla ya Love Island.
Love Island ni kipindi ambacho kinawaweka vijana wa kiume na kike katika nyumba moja (Villa) kwa miezi kadhaa kwa madhumuni ya kupata wapenzi na mshindi!
Watu wengi wametuma rambirambi zao kwenye social media na vile vile kulaumu media kwamba ndio zimechangia yeye kujiua kutoka na kumwandika vibaya kama Man beater, Paedophile, abuser na kadhalika.
RIP Caroline!