Mwendokasi hali ni mbaya

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Kama kuna abiria aliyetoka na treni ya saa kumi namoja jioni kwenda Moro kashafika na kaoga kapumzika huwezi amini hapa kivukoni watu wapo tokea saa 10 hamna magari

Yaani abiria wa Moro kafika na kashalala mtu wa kimara haelewi hadi sasa ataondoka saa ngapi

Sijui Serikali mna mpango gani na huu usafiri mnajinadi kila siku mmefanya makubwa mbona hali tete sana huku
 
Huo usafiri umeoza mkuu, usijichanganye kupanda utajuta , magari ni machache sana watu ni wengi mno
 
We ni mbuzi kweli aliekwanbia wanaopanda mwendokasi hawana hela ni nani

Mwendokasi ndio usafiri umewafanya watu kuacha magari kukimbia foleni na uchovu usijidanganye
Mbuzi ni yule uliemuacha kwako! Narudia Tafuta hela huwezi kusema una hela ukae kuanzia saa 10 ukisubiri mwendo kasi mjazane kama kuku kwenye tenga
 
 
Unaweza kufikiria huko maofisini hamna watu, ila kuna wanaume na wanawake walioenda shuleni wakapata elimu na kuondoa "ujinga", bahati mbaya waliongeza ujinga ndio maana wapo kwenye nafasi zao ila they don't give a shyte what's happening to their people.

Ukiuangalia mradi wa mwendokasi ndio utaamini sisi ni duni wa kufikiri na kutenda.

Hivi management ya mwendokasi inakaa ofisini kufanya nini? They piss me off big time.
 
Lengo lao wauze mradi kwa watu wao, haya mateso ni kujaribu kushawishi wananchi
Mawazo ya pingapinga Fc ya hovyo sana. Hakuna mtu mwenye mawazo eti ili wauze mradi basi watese kwanza wananchi, Chadema mkipewa nchi mna njia za hovyo sana kuhalalisha uhujumu uchumi.
No reforms no elections.
 
Asante Mungu kunipumzisha na mateso haya ya hayo magari
Mida kama hii naambaa kwenye Panton huku nikiwaza foleni ya mwendokasi hapo Kivukoni.
 
Hapa wanatafuta sababu ya kumpa mwarabu. Wanatesa raia ili wakimpa mwarabu kila mtu aseme ni bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…