Mwendokasi hali ni mbaya

Mwendokasi hali ni mbaya

Haka kanatoa suluhisho la hiyo changamoto

View attachment 3252467
Anakula AC huku akichungulia nje abiria wanavopigana vikumbo kuingia.Huku akisema moyoni daah kuna watu wanashida hii DSM si warudi vijijini ona wanavobanana kama kuku kwenye tenga..wanashindwa kununua hata ka Passo, Ist..

Huku akismile na kula Ice cream ya maziwa(kulainisha koo) za azam na kusikiliza Jana na Leo ya Wasafi fm mida ya kurudi home au Akila ngoma la CALIFORNIA DREAMING la PAC mwenyew mdogo mdogo
 
Hii ngozi nyeusi ni shida. Imagine mradi unakufa kisa kuzidiwa na wateja. Scandinavia, Japan, Germany au kwingineko ko kote itakuwa kashfa ya Karne. Huku kwetu it is OK as long as watu wanakula kulingana na urefu wa kamba zao.

Unakuta jitu boya limekaa pale halafu linakwambia eti "kaa pembeni sina chenji". Yaani unatamani ulirukie ulirarue lakini unashindwa. Are we a failed state or just a shithole country/people/race?🚮
Inasikitisha sana mkuu, huwa nikitumia huo usafiri naiwazia sana hii nchi. Huenda muda wetu wa kuwa civilised haujafika.
 
Pandeni bajaji
Na aliyeruhusu bajaj kuja mjini ndiyo kaharibu kabisa. Angalia zinavyopaki ovyo na kusababisha msongamano barabarani. Hizi zilitakiwa ziishie bara bara za mitaani tu siyo trunk roads. Ukizingatia ukosefu wa ustarabu kwa madereva wa hivyo vibajaj huwezi kuelewa kwa nini vinaruhusiwa kuingia mjini kati
 
tanzania bhana eti biashara au mradi wa mwendokasi unakufa kisa umezidiwa na wateja wengi ajabu..wakati uwingi wa abiria ndio fursa ya kuvuna mamilioni kama faida toka kwa wateja kiasi mradi ungeweza kujinunulia mabasi yake mapya wenyewe kwa faida itakayovuna..ila ndio hivyo vilaza wamekaa tu ofisini hawana mbinu wala mikakati ya biashara zaidi ya kuhesabu tarehe mwisho wa mwezi wapokee mshahara..ni ajabu la dunia biashara kufa kisa imezidiwa na wateja duuh hivi hawaoni aibu hao maboss wa huo mradi sijui wameajiriwa kwa kazi ipi zaidi ya hayo mabasi.!
Boss karidhika na kipato, hajali kinachosababisha apate hicho kipato. Na mfumo wa utendaji kwa TZ hasa serikalini, maoni ya mtumishi wa chini hata yakiwa mazuri na ya manufaa, ili kufanyiwa kazi lazima kwanza itafutwe namna kuonesha maoni kayatoa boss hayajatoka chini!
 
Kama kuna abiria aliyetoka na treni ya saa kumi namoja jioni kwenda moro kashafika na kaoga kapumzika huwezi amini hapa kivukoni watu wapo tokea saa 10 hamna magari

Yaani abiria wa moro kafika na kashalala mtu wa kimara haelewi hadi sasa ataondoka saa ngapi

sijui Serikali mna mpango gani na huu usafiri mnajinadi kila siku mmefanya makubwa mbona hali tete sana huku
Hilo ni tatizo la kutengenezwa ili malengo yao yatimie! Amka!!!
 
Kama kuna abiria aliyetoka na treni ya saa kumi namoja jioni kwenda moro kashafika na kaoga kapumzika huwezi amini hapa kivukoni watu wapo tokea saa 10 hamna magari

Yaani abiria wa moro kafika na kashalala mtu wa kimara haelewi hadi sasa ataondoka saa ngapi

sijui Serikali mna mpango gani na huu usafiri mnajinadi kila siku mmefanya makubwa mbona hali tete sana huku
Chini ya ccm hakuna kitu kotakachosimama.....sgr nimeipa Lifespan ya 10yrs
 
We ni mbuzi kweli aliekwanbia wanaopanda mwendokasi hawana hela ni nani

Mwendokasi ndio usafiri umewafanya watu kuacha magari kukimbia foleni na uchovu usijidanganye
Huwezi kuwa na gari ukang’ang’ana na mwendo kasi mzee acha porojo. Yani ungefungua mioyo ya abiria wa mwendokasi ungestaajabu kwamba 80% yao wanatamani leo kesho wangemiliki usafiri binafsi.
 
Wewe ni kenge hapo kariakoo watu wana pesa na wanakaa mbezi na wanapanda mwendokasi sio kila Tajiri anapanda boda boda jichanganye uzani kila mtu kwenye mwendokasi maskini
Utakuwa ni wendawazimu mtu eti ni tajiri halafu ahangaike na mwendokasi wakati bolt ipo! Tajiri anathamini afya yake kuliko kitu chochote, hakuna usalama kiafya ukipanda mwendokasi. Mtu mmoja mwenye homa ya ini anaweza ambukiza makumi ya watu mule kupitia kupakana majasho tu.
 
Lissu Akiingia madarakani hili suala asilifumbie macho afumue uongozi wote tuanze upya.
 
Ni kweli mkuu! Kuna watu wengi sana nawafahamu pale Kariakoo na wengine ni jamaa zangu wana biashara zao kubwa tu na hela wanazo kama uchafu lakini huyooo unamkuta kwenye Mwendokasi. Ni usafiri mzuri sana sema mipuuzi ya CCM imeshindwa kuusimamia!
Mi nawaona wapumbavu tu hao unaoita matajiri.
 
True kaka mimi mwenyewe nawajua kama jirani yangu ana maduka mawili ya nguo yule ni bilionea ana pesa vibaya ila kila jioni na mkewe utawaona wanasubiri mwendokasi za mbezi hawana makuu na boda hawataki hata kuziskia maajali
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 waambie kuna homa ya ini
 
Najiulizaga sana; hivi viongozi hawainagi AIBU kwa kufeli mradi kama hu? Yaani hawaoni aibu kabisaaa yaani? Interesting
 
Huo usafiri ukizingatiwa ni suluhisho la kudumu la foleni, njia yao haina foleni kwanini wakati wa jioni na asubuhi muda ambao abiria huwa wengi gari zisiongezwe vituoni??

Kama ilivyokua pale ferry kwenda kigamboni kipindi cha nyuma, MV kazi na MV kigamboni zilikua zinapiga kazi mchana ila asubuhi na jioni mv magogoni kale kakivuko kadogo ka zamani nako kanazama mzigoni kuokoa jahazi, ilikua hukai muda mrefu kusubiri kivuko, watu wakipungua kile kivuko kidogo cha zamani kinapoa zile mbili zinaendelea kupiga kazi.

Wangeiga huo mfumo, asubuhi na jioni gari zimwagwe za kutosha.
 
Hii nchi kila jambo ni jambo, Sasa hapo wananchi wanavoteseka na usafiri wao unakuta wanufaika wa huo usafiri wanasikia rahaaaa!
 
Katika hii Dunia hakuna mtu anapenda shida mazee! wale wote unao waona mabinti, mababa, wamama, e.t.c hawaupend huo usafiri ni shida tu.
 
Mbuzi ni yule uliemuacha kwako! Narudia Tafuta hela huwezi kusema una hela ukae kuanzia saa 10 ukisubiri mwendo kasi mjazane kama kuku kwenye tenga
Acha badi dharau kuwa na uhakika wa safari zako usione wengine wasio na uwezo wamependa!!!
Unaweza kukuta hata milioni kumi za dharura huna !! Mijitu kama nyie kichwani hamnazo!!!!
 
Hii ngozi nyeusi ni shida. Imagine mradi unakufa kisa kuzidiwa na wateja. Scandinavia, Japan, Germany au kwingineko ko kote itakuwa kashfa ya Karne. Huku kwetu it is OK as long as watu wanakula kulingana na urefu wa kamba zao.

Unakuta jitu boya limekaa pale halafu linakwambia eti "kaa pembeni sina chenji". Yaani unatamani ulirukie ulirarue lakini unashindwa. Are we a failed state or just a shithole country/people/race?🚮
Kwa nini hawatoi elimu kwa wananchi kuwa kuna mwendokasi app na unaweza kutumia simu yako tu ukaingia kituoni.
Hawatoi elimu ili wapate hiz chenji.
Mimi toka nimejifunza kutumia Application yao hayo mambo ya chenji nishasahau. Naweka hela na bar code ya kuscan inakuja.
Sijui kwa nini watu wananunua hata makadi wakati wana smartphone na bando
 
Back
Top Bottom