DOKEZO Mwendokasi Kivukoni-Kimara imezidiwa, daladala ziruhusiwe

DOKEZO Mwendokasi Kivukoni-Kimara imezidiwa, daladala ziruhusiwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Aisee najua watz wengi wenye maisha ya kawaida hutumia usafiri huu ili kupunguza gharama za maisha. Njia ya Kivukoni - Kimara ina bajaj lakini bado mwendo kasi ni vita ya kufa na kupona ambapo hali hii sio tu ni madhara kwa watumiaji bali pia kwa magari yenyewe na miundombinu.

Inaonekana kabisa magari yamezidiwa hadi kwa sasa watu wanapanda hadi milango haifungi, watu wanapitia madirishani kiasi cha kuharibu vioo. Sijui barabara kama zitakaa salama kwa hiyo overloading ya kila mara.

Suala la haya magari ni failure kwa kuwa hadi sasa inaonekana kuna magari machache, nadhani pamoja na uwepo wa bajaji, daladala ziruhusiwe ili kupunguza shida hiyo.

Aidha kuwe na mipango ya muda mrefu ili barabara isiwe inakuwa repaired mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom