KERO Responded Mwendokasi kutouza kadi siku za Wikiendi siyo sawa, abiria wanapata changamoto

KERO Responded Mwendokasi kutouza kadi siku za Wikiendi siyo sawa, abiria wanapata changamoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2025-08-02_16-02-47.jpg
Mwendokasi upande wa DART, kuna changamoto ya uuzaji wa kadi, kwa sasa mfumo ambao unatumika ni wa kutumia kadi kununua tiketi lakini wao wametoa maelekezo kuwa hawatakuwa wanauza kadi siku za weekend, na ni kweli taarifa hiyo wameitekeleza.

Abiria wanapata changamoto tangu 26 Julai 2025, abiria wengi hawana kadi, maafisa usafirishaji wa UDART wanajitahidi kuwaelekeza abiria kusaidiana ili wasafiri.

Hivi wanadhani kwamba wateja wao ni walewale wa siku zote? Hawajui Jiji la Dar es Salaam lina watu wapya kila siku, sasa unapoondoa uuzaji wa kadi Wikiendi maana yake hawataki watu wapya watumie huduma hiyo?

UDART suala la kuuza kadi inapaswa iache kazi hiyo impatie UDART kwa sababu, UDART ndio anafanya masuala ya FARE COLLECTION, DART anang'ang'ania kitengo hicho kwa maslahi yao ya kukuumiza UDART

Naomba kuwasilisha.

DART NI UOZO.
photo_2025-08-02_16-02-34.jpg

photo_2025-08-02_16-02-36.jpg

photo_2025-08-02_16-02-40.jpg

photo_2025-08-02_16-02-43.jpg

Ufafanuzi wa DART upo hapa ~ DART: Sio lengo letu kuuza kadi za Mwendokasi siku za 'weekend'

Pia soma ~
Abiria tukienda kununua kadi za Mwendokasi tunaambiwa zimeisha
 
Back
Top Bottom