Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Samahani Leo nimeamka sio poa!
Unafika kivukoni mabasi sita yamepaki mnasubiriwa mjazane dakika ishirini nzima mmekaa tu mmejaa hasira Kali eti mnasubiri bus na mnayaona yamepaki hatimae ghafla wanaachia basi moja la kimara wote mnakimbilia spidi kali kupanda kama wanyama pori manyumbu wengine mnapamia wazee wanaanguka mnaombana samahani.
Wengine wanaangusha cm na pochi hawajui masikini akili iko kwenye kuwahi siti dirishani basi abiria mnajazwa kama nyanya bus linaondoka humo ndani kuna harufu Kali mmejaa kama nyanya mtu hata kuhema mtu huwezi umebanwa hugeuki ukikaa vibaya unaibiwa cm na pochi! Halafu pale kuna Mgambo wa darasa la nne wanafokea watu na PhD zao, wanakwambia wewe panga mstari haraka uingie kwenye bus alaaa!
Saa zingine mara uko fire gari zinàkuja za kwenda kimara watu wamejaa hata mlango haufunguki gari ikifika fire ukiwaangalia abiria walioko ndani wamebanwa wametoa macho kama mijusi imebanwa na mlango wanapumua kwa shida majasho yanawavuja bàlaa wote wamekunja uso zao! Na hawataki wewe uingie!
Sasa Pale fire asubuhi labda unaumwa sana Sasa unasubiri bus la kwenda Muhimbili utakaa pale nusu saa nzima bus haliji mpaka unazidiwa na unaweza kudedi kama vipi eti mpaka mjazane kwanza ndo wapige cm eti mara ghafla utaona wanaleta bus moja tu mjazane kama nyanya mara wagonjwa wangine wako hoi!
Ukiwauluza kwanini mabasi ya Muhimbili ni machache sana asubuhi saa zingine wanasema eti trafiki wa fire akiconcerntrate kuruhusu magari ya morogoro road tu basi mabasi yanayotoka Muhimbili kwenda Gerezani yanakwama kwenye foleni na kusababisha uhaba wa mabasi ya kwenda Muhimbili. Basi wanaohusika please mwambieni yule trafiki anazingua.
Kiukweli wenye wanaendesha huu mradi wa mwendokasi na viongozi waliowapa tenda wote wataenda jehannam maana si kwa kutesa watu hivi.
Kiukweli viongozi wengi wa Tanzania wanatesa sana raia wa nchi hii masikini. Watu wanateseka sana na inajulikana watesi wao wengi wakifa watafikia jehannam sababu wamejaa kiburi na viongozi wengi hudhani wataishi duniani milele kumbe wakifika miaka 70 tu wengi wao hufa kwa pressure na kupooza sababu ya kuwa na matumbo makubwa yaliyoshiba sukari iliyonunuliwa kwa Tozo za watu masikini. Hawa viongozi wakifa huwa Kuna dawa inaitwa Formalin wanapakwa Ili miili yao iliyokwisha kuanza kuoza isitoe harufu Kali. Nawakumbusha formalin inatusubiri duniani tunapita tu!
Idadi ya mabasi ni ndogo mno kulinganisha na abiria kama vipi mabasi yaongezwe asubuhi na jioni!
Nyie wababe UDART Wekeni route ya Kivukoni - Muhimbili kama vipi just for fun ikiwapendeza!
Good day!