Mwendokasi yaingia nchini Kenya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Baada ya Tanzania kuwa na mradi wa mabasi ya mwendokasi( DART) hatimaye wivu wa maendeleo umeikumba nchi ya Kenya kwa kuleta mabasi mapya ya mwendokasi.

Mabasi hayo ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 130 yatasaidia kupunguza adha ya usafiri wa umma, na kusaidia pia kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji.

Source :Citizen
 
Kuiga maendeleo si ndio ujanja wakuu...na sisi tuige yao mazur
Na sisi tungewaiga kushinikiza mpaka kupatikana katiba mpya tungekuwa wa maana kweli. Lakini akili zetu wa Tanzania zinaishia kulinganisha size za tupu zetu na wakenya hapa jf. We are a gone case kuanzia nchi yeneyewe mpaka wananchi wake.
 
Ni kweli hamna barabara maalum kama ilivyo Dar es salaam

Na wengi wamehoji hilo

Tatizo umekimbilia kuposti baada ya kuona picha, bila hata kushirikisha ubongo na kujifahamisha kwanza nini kinaendelea. Sasa utaishia kuulizwa maswali na ukose majibu maana huna uelewa wa nini hicho ulichopost.

Haya hapa ni mabasi ya kampuni binafsi na wala haihusiani na mambo ya mwendo kasi au mfumo wa DART. Ni kama jinsi leo hapo Dar mojawapo ya makampuni ya daladala waamue kutumia mabasi yaliyounganishwa na kuyaingiza mjini, daladalaa zenye uwezo wa kubeba abiria 130 kwa mpigo.
 
Mi natamani tuige wakenya tuitoe ccm na tupate katiba mpya

Dah CCM yenu kuitoa sidhani kama itakua rahisi kihivyo, nimepitia mada zenu za siasa, naona polisi wenu ni mikwara full kwenda mbele. Yaani polisi wa kuzuia maandamano ya raia wa kawaida wanapita pita mijini huku wamevaa full commando kama kwamba wamejiandaa kwa vita maalum.
Mapicha ya kuogofya bana, hadi nimejikuta nashukuru sana nchi yangu na uongozi wake na hulka yetu kama Wakenya, tuna tofauti zetu lakini kukaliwa design hii ni noma.

Kuna jamaa kaanzisha hii mada huku Jeshi la Polisi: Mazoezi yanayoendelea ni ya kawaida, hayalengi kuzuia shughuli zozote halali

 
Wewe jamaa ni kichwa maji kweli,
Thread yako umeita mwendokasi, halafu kwenye hii comment unasema hazihusiani na mwendokasi,
Sasa si ungesema tu ni daladala kama uda za ubungo mbagala.
Uache uvivu wa kufikiria.
 
Hizo ni daladala tu kama zile uda za mnazi mmoja - kivukoni,
Huwezi fananisha na modernised udart.
 
Mkuu kwani yakiwa ya watu binafsi haruhusiwi kuwekewa barabara maalum..!?

Sema basi kuwa yatapita kwenye Bay pass, nyingi hamkosei jambo,mbona mtapozindua miradi mbalimbali ya maendeleo tunawapongeza.. acha hizo wewe.
 
Mkuu kwani yakiwa ya watu binafsi haruhusiwi kuwekewa barabara maalum..!?

Sema basi kuwa yatapita kwenye Bay pass, nyingi hamkosei jambo,mbona mtapozindua miradi mbalimbali ya maendeleo tunawapongeza.. acha hizo wewe.

Daladala za mtu binafsi haziundiwi barabara maalum, sioni itakua vipi hapo. Barabara tunazo, kuna zingine tumeanza hata kujenga juu, sasa hamna haja ya kutenga barabara kwa ajili ya mabasi ya mtu binafsi.

Ukija Nairobi utakumbana na mambo kama haya, sana mbona tuwe na barabara maalum?

 
Wewe jamaa ni kichwa maji kweli,
Thread yako umeita mwendokasi, halafu kwenye hii comment unasema hazihusiani na mwendokasi,
Sasa si ungesema tu ni daladala kama uda za ubungo mbagala.
Uache uvivu wa kufikiria.

..Hapana mkuu hilo basi siyo sawa na daladala za mbagala, jambo ambalo hata wewe unalijua fika. Pili sisi tuna mabasi kama hayo hayo (ingawa model zaweza kuwa tofauti) ambayo yanatumia barabara zake hivyo hayakumbani na foleni. Hivyo haya si mabasi ya mwendo kasi bali ni mabasi.
 
Kukopi,na kupesti,ndio mimi nilisema,tusijilinganishe na wakenya,hawana cha mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…