Mwendokasi yaingia nchini Kenya

Hayo mabas sio ya mwendo kasi sababu hawana barabara ya mwendo kasi utayeaitaje ya mwendokasi??
 

Hapo tunawaonesha wakenya jinsi police walivyo imara. Hapo ni police tu bado wanajeshi hujawaona
 
Tuwe waungwana na kukubali kuwa majaa yametupita kwa mambo mambo mengi
Mfano wenyewe wameingiza barabarani mabasi kama yetu na pesa ambazo wangetumia kujenga miundombinu ya kutoka Kimara - Ferry kwa ajili ya mwendokasi pekee wenyewe wameitumia kujenga barabara za magari yote.
Sisi hapa nasikia tumetumia zaidi ya US $300 million kwa hii barabara isiyo cover hata 10% ya mji kwa ajili ya magari ya aina moja tu. Usije kushangaa Wakenya wametumia gharama hiyo hiyo au zaidi kidogo kuboresha barabara za mji mzima na kwa magari yote!
Kiukweli ukiangalia picha hiyo waliyoweka hapa unauona ukweli huu bila hata kusoma chuo kikuu.
Hizo ni daladala tu kama zile uda za mnazi mmoja - kivukoni,
Huwezi fananisha na modernised udart.
Kukopi,na kupesti,ndio mimi nilisema,tusijilinganishe na wakenya,hawana cha mno.
Hayo mabas sio ya mwendo kasi sababu hawana barabara ya mwendo kasi utayeaitaje ya mwendokasi??
 
Usichanganye hoja hapa mada ni mabasi ya mwendo kasi sio gharama wala superiority ya Tanzania au Kenya.

Kwa kipengele tu cha kukosa independent routes kwa hayo mabus hayawezi kuwa ya mwendokasi hayo mabus yapo kwenye jam na magari mengine ya kawaida yanashare the same roads unasema ya mwendokasi?
 
Na hapo ndipo tunapokwama kama taifa. Huwezi kuongelea kitu kimoja bila kuongelea vitu vinavyokitengeneza, mwishowe utaishia kumuona chui mkali lakini ukimchunguza unagundua ni picha ya chui kwenye karatasi!
Hivi unadhani ni muda gani utakuja kuongea gharama, efficiency, running costs nk kama sio hapa!? Au utaishia kuwa kama mtoto mdogo ambaye akiona logo ya NMB popote anasema ni mwendokasi!
 
Sema mabasi makubwa marefu yaingia Kenya hayo mabasi kuyaita ya mwendokasi ni sawa na kuita mkokoteni pickup.

Najua kuna ufisadi mkubwa darts from the scratch lakini kiite kijiko kijiko sio beleshi dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…