Uchaguzi 2020 Mwenendo wa ushindi Kiti cha Urais toka Mwalimu Nyerere hadi Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Mwenendo wa ushindi Kiti cha Urais toka Mwalimu Nyerere hadi Dkt. Magufuli

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
1965-Mwalimu JK Nyerere alishinda kwa kura 2,520,904 sawa na asilimia 96.46

1970- Mwalimu JK Nyerere alishinda kwa kura 3,220,636 sawa na asilimia 96.7

1975- Mwalimu JK Nyerere alishinda kwa kura 4,172,267 sawa na asilimia 93.25

1980- Mwalimu JK Nyerere alishinda kwa kura 5,570,883 sawa na asilimia 95.50

Mwaka 1984 Mwalimu aliamua kung"atuka akiwa bado na nguvu

1985- Mzee Aly Hassan Mwinyi alishinda kwa kura 4,778,114 sawa na asilimia 95..68

1990 Mzee Mwinyi alipata kura 5,196,120 sawa na asilimia 97.78

Mwaka 1990-1992 vuguvugu la vyama vingi likaanza likiungwa mkono na Mwalimu aliyeamini mawazo Mbadala ya wachache yanaweza yakaliponya taifa kuliko mawazo yanayofanana ya chama kimoja, Niwakumbushe vijana.....WANA CCM WENGI WALIMPINGA MWALIMU KWENYE HOJA YA VYAMA VINGI.

1995- Benjamin W. Mkapa alishinda kwa kura 4,026,422 sawa na asilimia 61.82

2000- Mzee Mkapa awamu ya pili akashinda kwa kura 5,863,201 sawa na asilimia 71.74. Uchaguzi huu ulitia dosari nchi kwa mauaji yaliyotokea Zanzibar. Rejea kitabu cha Mkapa

2005- Mzee Kikwete alishinda kwa kura 9,123,95 sawa na asilimia 80.28 ya kura zilizopigwa.

2010- Mzee Kikwete alishinda kwa kura 5,276,827 sawa na asilimia 62.83

2015- Mzee John Magufuli alipata kura 8,882,936 sawa na asilimia 58.46

2020- Mzee John Magufuli amepata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.40

Mwisho, Idadi ya wapiga kura waliojitokeza kwenye uchaguzi wa 2015 ilikua 15,596,110 kati ya wapiga kura 23,161,440 walioandikishwa. Mwaka 2020 wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29,754,699 na waliopiga kura 15,091,950 pungufu ya wapiga 504,160.

Jukumu letu wazee nikuwakumbusha vijana tulipotoka, jukumu la viongozi wa dini ni kukemea maovu, jukumu la wanasiasa nikusimamia sheria si kuzipindisha. Jukumu la Watanzania nikuipigania nchi yao wakiamini hakuna nchi nyingine wenye hati miliki nayo isipokua Tanzania.

TIMIZA WAJIBU.
 
Chaguzi za Nyerere na Mwinyi enzi za chama kimoja hazihesabiki!

Ule ulikuwa ni utani!
 
2020 kulikuwa hakuna uchaguzi. Sijui kwann epoteza muda kuandika habari za 2020??
 
Hujui hata mashataka ya kupelekwa ICC unaelimu ndogo ya mambo ya kidumia
 
wana ccm wameshinda sasa wanaandika historia ya nini wakati enzi mwalimu na mwinyi kulikuwa na chama kimoja? ilitakiwa historia ianzie kwa mzee mkapa
 
Wasichojua wengi ni kuwa watanzania kama sehemu ya wakazi wa dunia hii wameishapiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko wakati wowote. Wana taarifa zote na wanafahamu chochote wanachofahamu watu wa ulimwengu huu tena kwa wakati ulio sawia kabisa.
 
... wakati enzi mwalimu .... kulikuwa na chama kimoja? ilitakiwa historia ianzie kwa mzee mkapa
Una uhakika, Mkuu?
===
Three political parties participated in those elections namely, Tanganyika African Union (TANU), United Tanganyika Party (UTP) and African National Congress (ANC).However, only TANU won in some constituencies to become the first party to have members in the Legislative Council.

 
ikumbukwe kuwa nchi ilikuwa ndio kwanza ilikuwa inajiondoa kutoka kwenye makucha ya ukoloni mkongwe,chaguzi zake zilikuwa na sura ya ukombozi tofauti na huu uliotia fora kwa uhuni
 
Back
Top Bottom