Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
[Mahakama imeanza.]
[Karani anasoma kesi ya Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025.]
[Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.]
KATUGA: Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, naitwa Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mkuu.
Nipo pamoja na:
1. Job Mrema, Wakili wa Serikali Mkuu;
2. Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali Mkuu;
3. Tawabu Issa, Wakili Mwandamizi;
4. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali;
5. Winiwa Kasara, Wakili wa Serikali.
KATUGA: Waheshimiwa Majaji, jopo hili la Mawakili sita linaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili leo.
[Mshtakiwa yupo Mahakamani na anajiwakilisha mwenyewe.]
KATUGA: Shauri limekuja kwa ajili ya Mshtakiwa kuwasilisha hoja zake. Upande wa Jamhuri tupo tayari.
JAJI NDUNGURU: Mshtakiwa?
LISSU: Nipo tayari.
JAJI NDUNGURU: Tuendelee. Nakumbuka jana tuliishia pale ulipotaka kuanza hoja ya tano.
LISSU: Waheshimiwa Majaji, nalazimika kujitetea mwenyewe.
Nipo gerezani mwaka mmoja na nusu.
Kile ambacho tungetumia muda wetu vizuri kukitumia kwa mwezi mmoja, nalazimika kutumia muda wangu wa final submission kwa wiki moja.
Kama kuna jambo nimelisahau jana, nitalirudia.
Nataka nianze. Yapo baadhi ya masuala jana niliyasahau.
Ndiyo ilivyo hivyo. Nalazimika kufanya kazi ya mwezi mmoja kwa wiki moja.
JAJI NDUNGURU: Tuendelee.
LISSU: Kuna kitu muhimu juu ya hoja niliyoimaliza nayo jana.
Je, maneno yanatengeneza uhaini?
Nataka niongee kitu muhimu ambacho kitasaidia Mahakama inielewe na kufanya uamuzi sahihi sana.
Kwa nini Mahakama ya Rufani katika Khatibu Ghandi ilisema, “Maneno matupu hayavunji mfupa”?
Mere words do not constitute treason.
Ni kwa sababu Mahakama ya Rufani ilikuwa inafahamu historia yetu kuhusu uhaini.
Na msiwe na wasiwasi, sitotumia masaa matatu katika hilo.
Sheria yetu ya Jinai (Penal Code) ilitungwa mwaka 1930.
Na sheria yetu ilitungwa moja kwa moja kutoka Uingereza. Waingereza walikuwa wanatutawala.
Mwaka mmoja kabla ya 1929, that is, Bunge la Uingereza lilipendekeza sheria za jinai kwa ajili ya Tanganyika, Kenya, Uganda na Nyasaland, modern-day Malawi.
Bunge la Uingereza lilipendekeza sheria za jinai.
Ndiyo, mwaka 1930 Bunge la Uingereza likatunga sheria kutokana na draft ya Westminster.
Vifungu vinavyohusu uhaini vilichukuliwa moja kwa moja kutoka katika sheria ya Uingereza ya mwaka 1848.
Hiyo sheria ya Uingereza inaitwa Treason Felony Act ya 1848.
Palikuwa na tofauti moja na sheria hiyo ya Treason Felony Act.
Kwenye ile sentence inayosema, katika kifungu cha 39(2)(d), kwenye sheria ya Uingereza inasema:
“manifest such by publishing any writing or printing or by open advice speaking or by any overt act or deed.”
Sasa, Waheshimiwa Majaji, sheria ya Uingereza ya mwaka 1848 ilikuwa imeweka uhaini kwa kuzungumza, kwa kutoa maneno.
Sasa, hicho kifungu kilichokuwa kinaruhusu maneno kuwa ni sehemu ya kosa la uhaini kiliwekewa ukomo wa maisha yake.
Ile sheria, kifungu chake cha 4, kilisema hicho kifungu kitatumika kwa miaka miwili tu.
Kwa hiyo, baada ya mwaka 1850, kifungu hicho kiliacha kutumika kama sababu ya kumtia mtu hatiani.
Na ilipofika mwaka 1891, the British Parliament amended that section by repeal.
The repealing Act was the Statute Law Revision Act of 1891 of Westminster.
From that time to this day, English law to treason is counted as section 39 of our Penal Code.
Our Penal Code was enacted in 1930 by British law.
Kwa vile English law ilishafuta uhaini wa maneno, ndiyo maana sheria yetu vilevile haijawahi kuwa na uhaini wa maneno.
Na ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, Marehemu Jaji Mkuu Francis Nyalali kwenye Khatibu Ghandi alisema kuwa maneno matupu hayafanyi uhaini.
Alikuwa anajua hii sheria imetoka wapi.
Waheshimiwa Majaji, nimesema hiyo sheria ya uhaini kama iliyopendekezwa na Uingereza kwa Tanganyika, Uganda, Kenya na Nyasaland.
Isipokuwa nchi moja imeongeza uhaini wa maneno.
Uganda katika Penal Code yao wameongeza uhaini baada ya Mwingereza kuondoka.
Kwa sheria yetu hakuna uhaini wa maneno.
Napendekeza uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza, Regina v Her Majesty's Attorney General (Appellant) ex parte Rusbridger and another (Respondents).
Wanataka kuingiza kitu kwenye kesi hii wakati Waingereza waliotuletea sheria hii waliachana nacho tangu 1890; wao wanataka kukileta leo.
Pia lengo la upande wa mashitaka ni kuingiza uhaini wa maneno katika sheria zetu ambao haujawahi kuwa katika sheria zetu milele.
Na tatu, hoja hii ya upande wa mashitaka inapinga msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye Khatibu Ghandi kwamba maneno matupu hayatengenezi uhaini.
Rai yangu, Waheshimiwa Majaji, mtakapofanya uamuzi msikubali mwaliko wao wa kuingiza katika sheria yetu ya uhaini mambo ambayo hayajawahi kuwepo kabisa.
Mambo ambayo Mahakama ya Rufani ilishayawekea msimamo.
You are bound by what Court of Appeal said: “Uhaini wa maneno haupo.”
Sasa, kwa ridhaa yenu, Waheshimiwa Majaji, naomba nizungumze suala la PUBLICATION.
Suala ni, je, Mshtakiwa anayelalamikiwa alichapisha katika mtandao wa Jambo?
Waheshimiwa Majaji, hili ni suala muhimu sana.
Ni suala la kufa au kupona kwa kesi.
Both in Khatibu Ghandi and Gray Likungu Mattaka, ili upande wa Mshtakiwa utiwe hatiani ni lazima upande wa Mashitaka uthibitishe printing or writing.
Na usipothibitisha, the case dies on his arrival.
Kwenye ukurasa wa 132 wa Rekodi, upande wa Mashitaka ulituhumu siyo tu kwamba Mshtakiwa alitoa maneno wanayoyalalamikia, bali pia alichapisha katika Jambo TV YouTube Channel.
Umma ukiyatumia hayo maneno mara moja.
Kuna kitu kimoja hapa nataka niweke wazi.
Upande wa Mashitaka hajanituhumu kuchapisha kupitia kwa mtu mwingine. Tuhuma yao ni kwamba nilichapisha mwenyewe.
Sikusaidiwa wala sikutumia mtu mwingine.
Kwa hiyo kusiwe na hoja kwamba, “Ah, ha ha, ukitumia fulani?” Hapana. Wanatakiwa wathibitishe wenyewe.
Waheshimiwa Majaji, hii publishing inayotajwa katika kifungu cha 39(2) cha Kanuni ya Adhabu, ambayo lazima ithibitishwe na upande wa Mashitaka.
Huu uchapishaji unaozungumzwa hapa ni uchapishaji wa namna gani?
The term “Publishing” or “Publication” is not defined anywhere in the Penal Code.
The fact kwamba haijatafsiriwa haina maana kwamba haijulikani.
Tafsiri yake, Waheshimiwa Majaji, ilitolewa katika Mahakama ya Rufani kwenye Gray Likungu Mattaka na hiyo decision ikawa affirmed na Khatibu Ghandi.
Kwenye ukurasa wa 509 hadi 510 wa Gray Likungu Mattaka, Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki ilisema:
“The term publishing under section 39(2) of Penal Code means sending out or sharing a writing or printing with third party.”
Na huo uamuzi ukawa affirmed by our own Court of Appeal in Khatibu Ghandi.
Kitu kisicho maandishi au chapisho kikisambazwa, hiyo siyo publishing kwa mujibu wa sheria.
Waheshimiwa Majaji, kama publish is sharing a writing or printing with a third party, what about a video clip?
Waheshimiwa Majaji, video pictures or television images are publication under the Cybercrimes Act.
Kwa bahati mbaya, sijashitakiwa under the Cybercrimes Act, yaani Sheria ya Makosa ya Mtandaoni. Kwa hiyo publishing ya sheria ya makosa ya mtandaoni ibaki hukohuko.
Waheshimiwa Majaji, the term publication includes, chini ya sheria ya vyombo vya habari, publication ina include usambazaji wa video.
Kwa bahati mbaya yao, sijashitakiwa chini ya sheria ya habari, kwa hiyo na hiyo publication ya sheria ya habari ifike hukohuko.
Waheshimiwa Majaji, nimeshitakiwa chini ya Penal Code ambapo publication ni writings or printing.
Na hiyo Penal Code ipo chini ya Katiba, chini ya Ibara ya 13(6)(c), ambapo sisi raia tunalindwa na Katiba kwamba hatuwezi kushtakiwa kwa makosa yasiyokuwepo kwenye sheria.
Kama hayakuwa makosa jana, hayawezi kuwa makosa leo.
Waheshimiwa Majaji, kwa heshima kubwa kwa Mawakili ambao wamekuwa wakipambana na mimi kwa mwaka mmoja na nusu, kesi yao ilikufa siku ilipowasili. Dead on arrival.
Kwamba mwaka mmoja na nusu tunajaribu kuthibitisha jambo lililotakiwa kujulikana siku ya kwanza.
Imenipa simanzi kubwa sana kuhusu mfumo wa haki jinai wa nchi yetu.
Mahakama zetu, Polisi wetu.
Waheshimiwa Majaji, twende kwenye ushahidi wao sasa.
Suala hili limekuwa mojawapo ya masuala yaliyojadiliwa vikali Mahakamani.
Kama nilivyosema, ilikuwa ni suala la kufa au kupona kwa kesi.
Ushahidi ukoje, Waheshimiwa?
Upande wa Mashitaka waliita mashahidi wao:
PW1
PW2
PW3
PW16
PW17
Upande wa utetezi, mashahidi wote watano walipinga jambo hili.
Tuanze na ushahidi wao.
One notable thing in particular, with exception of PW17, testified under oath that it was the accused who published a video on Jambo TV YouTube Channel.
Ulikuwa ni mkanganyiko mtupu.
Walijichanganya, wakachanganyikiwa.
Tuanze na PW1, George Bagyemu.
Waheshimiwa Majaji, kwenye ukurasa wa 144 wa rekodi, PW1 anazungumzia hiyo video.
Baada ya kuangalia vipande vipande vya hiyo video clip, aliamua kuwatafuta Jambo TV.
Maneno yanayofuata: “Who recorded the clip?”
Akiwatafuta Jambo TV walio-record hiyo video.
Kwa hayo maneno tu, hiyo video ilichapishwa na Jambo TV.
Ukurasa wa 144.
Na ukurasa wa 145 anasema alichoambiwa na Jambo TV kwamba anaijua/anaifahamu clip na kwamba hiyo imerekodiwa na mfanyakazi wake.
Anakubali mara ya pili kwamba aliyerekodi siyo mimi.
Anasema huyo mtu wa Jambo TV aliyerekodi yupo Dodoma.
PW1 alipiga simu kwa Kamishna wa Polisi Ng’anzi Dodoma kumjua aliyerekodi na eneo paliporekodiwa.
Kwa hiyo PW1 chini ya kiapo anasema aliyerekodi siyo mimi.
Yote hayo yalijulikana tarehe 6 Aprili 2025. Kwamba nani alichapisha hiyo video, tena siku tatu baada ya mkutano kufanyika.
Walijua vizuri nani alirekodi, ila kwa utaratibu wa Polisi wakasema, “Mpe kichwa.”
Waheshimiwa Majaji, tarehe 7 wakampata aliyerekodi hiyo video.
Wakapata na nakala ya hiyo video yenyewe.
Na tarehe 7 hiyo hiyo wakapata na maelezo yake aliyerekodi.
Maelezo ya PW17 yapo Mahakamani kama Kielelezo D16.
Akaeleza kinagaubaga jinsi alivyoagizwa na Boss wake, John Marwa.
Vifaa walivyokuwa navyo kama Camera Sony NHR 100.
Walikuwa watano.
Akaeleza walivyorusha moja kwa moja.
Akaeleza walivyopeleka kwenye mitandao ya Jambo TV kama YouTube, Instagram na X.
Akawaambia kwamba hajaziondoa; zipo mitandaoni hata sasa.
Hiyo ni tarehe 7, siku mbili kabla sijakamatwa.
Kwa sababu ya hayo, Polisi walikuwa na hamu ya kunikamata siku hiyo hiyo ya tarehe 7.
Walikuwa na ushahidi wa maandishi yake na memory card aliyokabidhi.
Baada ya siku mbili ndiyo wakanikamata kwa kuchapisha kwenye mtandao.
They are not even ashamed! Shame on you. Shame on you. Shame on you.
Maneno niliyoyasema yapo ukurasa wa 145.
Na katika ukurasa wa 147, “it’s the accused who published with the intention to threaten the executive.”
Mdomo mmoja, ndimi mbili.
Na katika cross-examination PW1 alikiri kwamba ilipelekwa mtandaoni na PW17.
Alikiri pia kwamba amesoma maelezo ya shahidi.
Hata hivyo, aliendelea kung’ang’ania ni Mshtakiwa ndiye aliyechapisha katika mitandao, ukurasa wa 159.
Waheshimiwa Majaji, PW1 aliendelea ku-flip-flop.
Ukurasa wa 160 anasema, “It’s not true a Jambo TV employee recorded a clip.”
Akasema siyo kweli kwamba PW17 aliyechapisha mtandaoni peke yake ni pamoja na Tundu Lissu.
Alipozidi kubanwa, akabadilika tena, ukurasa wa 165 hadi 166.
Akasema PW17 ndiye aliyeniambia yeye kuwa amechapisha.
Ndimi mbili kama nyoka. Nyoka ni hatari.
Waheshimiwa Majaji, PW1 aliulizwa alikuwa ana maana gani aliposema kwamba ni PW17 ndiye aliyechapisha.
Akasema, “Tumechapisha sisi ila yeye ndiye aliyesababisha.”
Akaulizwa alikuwa na maana gani kusema Jambo TV ndiyo waliochapisha.
Akasema, “Nilikuwa na maana kwamba ni Mshtakiwa ndiye aliyesababisha Jambo TV kuchapisha.”
Pia ni maneno ya Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga, kwamba nilichapisha kupitia kwa wengine.
Waheshimiwa Majaji, huo ndio ulikuwa ushahidi wa PW1 na ndiye alikuwa leading witness.
Evidence was totally lost credibility.
Waheshimiwa Majaji, twende kwenye ushahidi wa PW2, ukurasa wa 211 wa rekodi za Mahakama.
Ni confusion ile ile ya boss wake, George Byagemu.
PW2 katika ukurasa wa 214: “I don’t know who published video in Jambo TV.”
Huyu ni shahidi wa upande wa Mashitaka.
Anasema hajui nani aliyechapisha video katika mtandao wa Jambo TV.
Kwenye re-examination, ukurasa wa 222, Waheshimiwa Majaji, akasema ni Mshtakiwa aliyechapisha hiyo video katika mtandao wa Jambo TV.
Kwa sababu alialika waandishi wa habari.
Waheshimiwa Majaji, PW3 alikubali katika ushahidi wake hiyo video ipo katika mtandao wa Jambo TV.
Na akakubali kwamba aliikuta huko katika mtandao wa Jambo TV.
Ukurasa wa 276, akasema katika uchunguzi wangu sikugundua nani aliweka hiyo video katika mtandao.
Nilimuuliza kama inawezekana kujirekodi mwenyewe na wakati huo huo unarusha matangazo wakati unahutubia.
Akajibu katika ukurasa wa 277, akasema sijui kibinadamu kama inawezekana kujirekodi mwenyewe na wakati huo huo unarusha matangazo wakati unahutubia.
Wakamleta Amini Mahamba, PW16, kuja kuokoa jahazi lao.
Ushahidi wa PW16 upo katika ukurasa wa 466 wa rekodi.
PW16 alisema kwa majigambo yafuatayo:
“I testify it was you who published a video on Jambo TV.”
“It was you who transmitted a video in Jambo TV.”
“It’s you who circulated a video on Jambo TV channels.”
“It’s you who distributed the video on the Jambo TV YouTube platform.”
Nilipoanza kumshughulikia, hayo madai yakacollapse.
Ukurasa wa 467: “Sina uhakika kama wewe ni mfanyakazi wa Jambo TV.”
“Sina uhakika kama una password ya kutumia Jambo TV YouTube Channel.”
Akaendelea kusema, “Nimesoma maelezo ya PW1 kwamba alikuwa ni mtu aliyerekodi mkutano.”
Na kwamba PW1 ndiye aliyerusha matangazo.
Mwanzoni alikuwa anasema ni wewe, ni wewe.
Kwenye cross-examination akasema, “Sina hakika kama ni wewe.”
Ukurasa wa 467.
PW16 akaendelea kueleza Mahakama, Waheshimiwa Majaji, kwamba hata George Byagemu...
That the video was recorded and live streamed by Jambo TV employee.
Amin Mahamba anasema PW17 kwamba walielekezwa na Mkurugenzi wao, John Marwa, na kulivestream hotuba yako.
Mahali pengine PW16 alizungumzia kwa kirefu Inspector Andrew Chulu.
Nilipomuuliza kama amesoma maelezo ya Andrew Chulu, akasema:
“Nimesoma maelezo ya PW17 na Andrew Chulu,” katika ukurasa wa 469.
Katika maelezo yake, Askari Polisi Andrew Chulu na mwandishi wa habari wa Jambo TV wanasema ni waandishi wa habari wa Jambo TV ndiyo waliorekodi na kusambaza video katika mitandao ya Jambo TV.
Baadaye akabadilisha maelezo yake katika re-examination, ukurasa wa 466.
Waheshimiwa Majaji, niende kwa shahidi wao PW17.
Ni star witness wa kesi yao.
Yeye ndiye anaweza kusema kweli nina kosa au nimewekwa gerezani bure.
Maneno ya PW17, maelezo yake yapo katika ukurasa wa 490.
PW17 anasema yeye na wenzake walitumwa na boss wao kwenda Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, kwenda kutangaza mkutano.
Akaendelea kusema, “Tulipofika Makao Makuu ya CHADEMA, we were prepared to cover the meeting and livestreaming.”
“We used the camera footage to mainstream the meeting.”
Kwa kwamba walitumia mtandao wao Jambo TV kutangaza.
Na kwamba jina walilotumia kurusha matangazo ni Jambo TV.
Kwamba hilo wazo la kutangaza live lilikuwa la kwao wala siyo la mwingine, ukurasa wa 492.
Yote hii ni examination in chief.
Ya shahidi wao. Hapo alikuwa hajahojiwa na mimi hata kidogo.
Amekubali kila kitu.
Waheshimiwa Majaji, katika mashahidi wote 17, mashahidi 12 wa Mashitaka na 5 wa utetezi, alikuwa ni shahidi mwepesi zaidi.
Kama ni goli la kujifunga wenyewe, ni kosa la kumleta shahidi PW17.
Tena goli la kisigino.
Kwa jinsi huyu shahidi alivyojifunga wala hawakum-re-examine, the case was finito.
[Mahakama inacheka.]
Ushahidi huu unaiambia nini Mahakama?
Katika kesi ya Makonyo John @ Kibuna v Republic, ushahidi huu, Waheshimiwa Majaji, siyo wa kuaminika.
Hakuna Mahakama inayoitwa Mahakama ya sheria itatumia ushahidi huu.
Totally unreliable and completely not credible.
Na hii siyo kesi ya kuku; ni kesi ya uhaini, inahusu maisha ya watu.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa utetezi ukoje?
Ushahidi wa utetezi ukinyooka.
Ukurasa wa 592 ni ushahidi wangu. Nilisema everywhere waliorusha matangazo siyo mimi.
Na vilevile upo ukurasa wa 621.
Na ukurasa wa 622.
Ukaungwa mkono na DW2, DW3, DW4 na DW5.
Mashahidi wote wa utetezi walikuwa consistent kwamba waliorusha matangazo na kadhalika walikuwa wafanyakazi wa Jambo TV.
Walisema in chief na walisema wakati wa cross-examination.
Lakini kubwa kuliko lote, utetezi huu uliungwa mkono na PW17 aliyekuwepo katika mkutano na aliyerusha matangazo.
Waheshimiwa Majaji, nataka kufunga hoja hii kwa kusema machache tu juu ya sheria.
Hoja hii ya publication ya video images, nimesema mwanzo, haipo kabisa katika sheria niliyoshitakiwa nayo.
Nataka kusema masuala ya habari yanaongozwa na Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.
Mtu yeyote akitaka kujua nani anayewajibika katika kurusha matangazo ya redio na mitandao...
Kifungu cha 7(1) ndiyo kinachosema nani mwenye haki ya kuhariri na kusambaza hizo taarifa zinazorushwa katika televisheni.
Nani ana haki na hayo matangazo na nani anayamiliki.
7.-(1) Every media house and journalist shall enjoy the following rights-
(a) freedom to collect or gather information from different sources;
(b) freedom to process and edit information in accordance with professional ethics governing journalists; and
(c) freedom to publish or broadcast news.
Kwa kifungu hiki, ile nonsense inayoitwa Constructive Publication imekufa on arrival.
Kwa sababu mwandishi au chombo inayokusanya habari ndiyo yenye habari.
Hakuna Constructive Publication hapa.
Waheshimiwa Majaji, hapa sitaki kuzungumzia maumivu ya kukaa gerezani mwaka mmoja na nusu.
Ni simanzi, ni masikitiko yangu, ni kwa State Attorney kunishtaki kwa jambo ambalo halipo.
Ambapo siku ya kwanza wangeweza kuona hakuna kosa.
Na hii itaenda hadi kwenye compensation.
Wameniweka gerezani kwa hoja ya uongo.
Nina watoto na familia, nawekwa gerezani kwa kosa ambalo halipo.
Naishi kwenye kachumba ka futi sita wakati nina nyumba nzuri tu.
Wanatungia watu makosa ya uongo, kwa mimi ninayeburuza miguu kwa kutembea na risasi mwilini kwa nchi yangu nzuri.
I can imagine kwa watu ambao si wajanja kama mimi sijui wanafanywaje.
Wanajua sijatenda kosa tangu siku waliponíkamata. Kila mtu anajua hilo.
JAJI NDUNGURU: Tuendelee, nimeshaandika.
LISSU: Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema hoja ya sita ni NEGATIVE.
Hoja ya saba, Waheshimiwa Majaji, ni je, Serikali ilitishwa na hayo maneno?
Hoja hii inazungumzia matokeo ya nia ya kutenda uhaini, 39(2).
Waheshimiwa Majaji, huwezi kuona katika kesi ya Gray Likungu Mattaka.
Na watu wengi hawajui kwamba kesi ya Gray Likungu Mattaka ndiyo kesi ya Bibi Titi Mohamed.
Mwenyekiti wa kwanza wa UWT na mpigania uhuru wa nchi hii.
Ule mtaa unaoitwa Bibi Titi Mohamed ni huyu aliyeshitakiwa uhaini.
Tunaita Gray Likungu Mattaka kwa sababu ndiyo alikuwa Mshtakiwa namba moja.
Mahakamani ni mahala pa kuelimishana pia.
Kesi ya Gray Likungu Mattaka haikufika katika intention.
Na ndiyo maana juzi nimesema Mahakama hii ina nafasi ya kuweka historia.
Mahakama hii sasa inaweza kujielekeza katika kifungu cha 10(2).
Kama nia ni kutenda kosa, then matokeo yaliyokusudiwa kutendwa na nia hiyo lazima yasemwe na yathibitishwe kwa ushahidi.
Waheshimiwa Majaji, kwa maana hiyo upande wa Mashitaka ulitakiwa kuonyesha kwenye hati ya mashitaka inayotuhumu kwamba kulikuwa na nia ya kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Walitakiwa kuonyesha matokeo ya nia hiyo: Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.
Na walitakiwa kuonyesha katika information kwamba wakitakiwa kuleta huo ushahidi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.
Upande wa Mashitaka haukuonyesha kwenye hati yao ya Mashitaka, kwenye information.
Walifikiri unarusha mashitaka hivi, litakalompata na limpate.
Hawaku-plead katika mashitaka kwamba any particular showed how the Executive of the United Republic has been intimidated.
That failure to show the results, the case is defective.
Essentials of information must be shown.
Lazima uonyeshe vielelezo vya Mashitaka na usipovionyesha, hati ya Mashitaka ni batili.
Siyo tu kwamba hakuonyesha vielelezo kwenye hati yao ya Mashitaka, vilevile hawakuonyesha ushahidi wowote.
Kwa jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilivyotishika.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ipo katika Sura ya Pili ya Katiba.
Yote ndiyo inaelezea Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa na Rais.
Ndiyo Kiongozi Mkuu wa Serikali, ndiyo Amiri Jeshi Mkuu.
Akipaswa aje atoe ushahidi kama Serikali yake imetishika.
Mimi niliomba aitwe.
Walionishtaki wakapinga vikali na Waheshimiwa Majaji mkanikubalia.
Mimi, walionishtaki, nilitaka aitwe lakini hakuna.
Mimi nilijua kifungu cha 10(2) kinataka nini lakini hakuna.
Vilevile, Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina Makamu wa Rais na wakati ule anaitwa Philip Isdory Mpango.
Mimi niliomba aitwe. Upande wa Serikali ulipinga vikali, kwa hiyo hakuna na Waheshimiwa Majaji mliwakubalia.
Mtu wa tatu anayeunda Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati ule alikuwa anaitwa Majaliwa Majaliwa.
Yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali na Kiongozi wa Bunge.
Mimi niliomba aitwe lakini mkanikatalia.
Serikali inaundwa na Mawaziri. Hakuna hata Waziri mmoja ambaye amekuja.
Serikali inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali; hakuja.
Serikali inaundwa na Mkurugenzi wa Mashtaka; hakuja.
Serikali inaundwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lakini hakuna kiongozi hata mmoja kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyekuja.
Serikali inaundwa na Wakuu wa Vyombo vya Dola, lakini hakuna hata mmoja.
Niliomba afike hapa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, lakini Serikali wakapinga na Majaji mkawakubalia.
Mlinikubalia waje Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.
Kingai alikuja lakini alinikatalia kutoa ushahidi.
Kwenye rekodi hakuna hata mmoja aliyekuja kuthibitisha kama Serikali ilitishika.
Kama Serikali haikutishika, maana yake sina kosa.
Upande wa utetezi hatukuwa na burden yoyote kuthibitisha hili.
Burden ilikuwa yao, lakini wameshindwa kuthibitisha na hata kujaribu wameshindwa.
Tuna kesi ya uhaini na wale wanaosema tumeitisha Serikali hawajajaribu hata kuthibitisha, hata Mkuu wa Wilaya fulani.
Waheshimiwa Majaji, hawa nilio wataja kutofika kwao Mahakamani kuna maana gani?
Maana yake ya kutomwita, maana yake walizuia asije kwa sababu kesi yote imejengwa kwenye misingi ya uongo.
Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, naiomba Mahakama iseme wangekuja wangesema ukweli, ndiyo maana hawakuitwa.
More importantly, jibu la suala la saba, Waheshimiwa Majaji, can only be NEGATIVE.
Jibu la suala hili: Serikali haikutishwa.
Wangekuwa wametishwa wangeitwa Mahakamani.
Jibu la hili ni HAPANA, HAWAKUTISHIKA.
Naomba twende mapumziko, tutakuja kuzungumzia masuala mengine.
JAJI NDUNGURU: Upande wa Mashitaka mnasemaje?
KATUGA: Waheshimiwa, hatuna pingamizi, isipokuwa hatujajua ni saa moja au saa moja na nusu.
Tuombe Mungu amalize akirudi.
LISSU: Saa moja na nusu, Waheshimiwa Majaji.
LISSU: Off record ni kwamba nakesha usiku kufanya kazi hii.
Ninapoomba kupumzika kwa saa moja na nusu ni ili nipate kupumzisha mwili kidogo.
JAJI NDUNGURU: Kwa mengi hayo hayo, kwa leo tuishia hapa. Tuendelee siku ya Jumatatu saa 3:00 asubuhi.
[Majaji wanatoka.]