DOKEZO Mwenge umekuwa mwiba mkali kwa Walimu Wakuu Halmashauri ya Momba. Wanalazimishwa kutoa mchango kwa vitisho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
1. Mwalimu Mkuu asipotoa mchango wowote anatishiwa kuvuliwa madaraka au kunyanyaswa kwa jambo lolote lile.

2. DEO wa Halmashauri hii ni mtu wa kuwatishia tu walimu na kuwalazimisha kutoa michango bila utaratibu.

3. Posho ya Mwalimu mkuu imekuwa kama fimbo ya kuwachapia hao walimu wakuu na kupelekea kila mchango wanamtupia Mwalimu mkuu.

4. Je, kama Mwenge unatengewa bajeti sasa hizi pesa zinaenda wapi?

5. Je, kuna uhakika gani kama hizo pesa zinaenda kwenye mwenge ikiwa hakuna uwazi na ushahidi katika ukusanyaji wa hizo pesa?

6. Kwanini MAAFISA ELIMU KATA kutoka kila Kata wapewe kazi ya kukusanya hizi pesa badala ya michango hii kulipwa kwenye Akaunti ya Halmshauri kama kweli ni halali?




Pia soma
 
Kinachoshangaza sasa huo Mwenge wenyewe ni useless tu. Hakuna sababu ya kuwasumbua watu kuchangia kitu ambacho hakina tija yoyote ile kwenye dunia ya sasa.

I wish ningekuwa Rais! Hakika ningeamrisha mara moja ukawekwe kwenye jumba la Taifa la Makumbusho.
 
1.Kubisha kuchangia mwenge ni uhaini
2. Kuhoji kuhusu kuchangia mwenge ni uhaini
Uzalendo ni kuchangia mwenge kwa maendeleo ya taifa mwenge wa uhuru kwa jamhuri ya muungano wa tz
 
Na kwa taarifa yenu wote mnaohoji kuhusu mwege taarifa zenu tunazo watendaji wa kata mitaa wote wamechangia laki moja moja
 
ukute labda huo mwenge una dawa ya kupumbaza kila unapopitishwa ndo maana mwenge hauruki kijiji utapita nchi zima tunakuwa mazombi mambo ya kipuuzi yanafanywa na viongozi na hatuna cha kuwafanya.

mimi niko nchi jirani ndo maana akili zimenisogea nimeona niwashtue.
 
 

Attachments

  • IMG-20240729-WA0003.jpg
    26.9 KB · Views: 9
Ukiona hivyo basi Kifo cha Mwenge hakiko mbali.
 
 

Attachments

  • IMG-20240729-WA0001.jpg
    23.9 KB · Views: 8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…