Mwenge una Siri Gani? Viongozi Mwanza wanafanya miradi usiku kucha

Mwenge una Siri Gani? Viongozi Mwanza wanafanya miradi usiku kucha

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Mwenge wa uhuru tunavouchukulia inaweza ikawa tofauti na tunavyodhani. Nadhani viongozi wa mbio za Mwenge wanaenda ku report Kwa Rais mambo mazito, hawajali Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi n.k. Wao wakikuta mambo ya ovyo wanakulipua juu.

Mwenge kesho unaingia Ukerewe ila viongozi wanawasha taa usiku na mafundi wamalizie soko na miradi mingine

Mwanza mjini ndo hatari viongozi wa serikali wanahaha wakihofia Mwenge Huu utendaji wa kinafiki wanaoonesha Kwa Sasa ungekuwa hivi siku zote tungekuwa mbali. Sio tungoje mambo ndo viongozi wateule watoke maofisini.

Soma Pia: Toka nakua na mpaka sasa sioni faida ya Mwenge wa Uhuru
 
Waulize Malofa waliouweka hapa
1728315879444.jpeg
 
KIla halmashauri lazima ianishe miradi itakayofunguliwa na Mwenge. Kwa tafsiri kuwa mwenge hauji kuzurula bali kuchochea maendeleo!
Sasa miradi iliyopanga kuzinduliwa lazima iwe kwenye shape nzuri kuweza kuzinduliwa, vinginevyo haitazinduliwa na hii haitakuwa habari njema kwa viongozi wa halmashauri husika, wilaya na mkoa!
 
 
Back
Top Bottom