Mwenge wa uhuru kuzindua Miradi 52 ya Billioni 84 Kilimanjaro

Mwenge wa uhuru kuzindua Miradi 52 ya Billioni 84 Kilimanjaro

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jumla ya miradi 52 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 84 inatarajiwa kukaguliwa, kuzinduliwa au kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika katika halmashauri saba za mkoa wa Kilimanjaro kuanzia Juni 28, 2025

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Katika miradi hiyo, miradi 20 itawekewa mawe ya msingi, miradi 23 itazinduliwa rasmi na miradi 9 itatembelewa kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji

Aidha, baadhi ya miradi hiyo inahusisha juhudi za vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika shughuli za uzalishaji mali kama sehemu ya kuinua kipato na ustawi wa jamii.

Baada ya kumaliza ziara ya mkoa wa Kilimanjaro, Julai 5, 2025, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa kwa mkoa wa Arusha, kupitia Kijiji cha King'ori, Kata ya Malula, Wilaya ya Arumeru, kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake mkoani humo

RC Babu amesema maandalizi yote ya kupokea mwenge huo yamekamilika, na mkoa wa Kilimanjaro uko tayari kuonesha mafanikio ya miradi inayotekelezwa kwa kushirikiana na wananchi, serikali kuu, sekta binafsi, na taasisi za kiraia



​
Chanzo: JAMBO TV
 
Back
Top Bottom