PreGE2025 Mwenge wa uhuru unazindua, kutembelea na kukagua jumla ya miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.7 Mtwara DC

PreGE2025 Mwenge wa uhuru unazindua, kutembelea na kukagua jumla ya miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.7 Mtwara DC

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Ikiwa ni siku ya nane tangu kuanza kwa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 katika Mkoa wa Mtwara, leo Mwenge huo umefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo umeweka mawe ya msingi, kuzindua, kutembelea na kukagua jumla ya miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.7.

Mwenge wa Uhuru ulianza ziara yake kwa kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Nambeleketela, mradi uliogharimu shilingi milioni 59.7.

Baadaye, Mwenge ulielekea Kata ya Mkunwa katika makao makuu ya halmashauri hiyo na kuzindua mradi wa barabara za mitaani wenye thamani ya shilingi milioni 51.1.

Katika mchana wa leo, Mwenge pia ulizindua rasmi nyumba za watumishi wa afya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150.9.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi alieleza kuridhishwa kwake na ubora wa miradi hiyo. “Ndugu zangu wa Mtwara DC, binafsi na timu yangu tumeshuhudia miradi mingi yenye ubora wa hali ya juu. Mfano mzuri ni Shule ya Nambeleketela ambayo miundombinu yake inakidhi mahitaji ya wanafunzi wote,” alisema.

Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa barabara katika Kata ya Mkunwa, Ndg. Ussi alisema kuwa mradi huo ni kielelezo cha kasi ya maendeleo na aliwataka wananchi kuutunza kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Aidha, Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kukagua miradi mingine mitatu ambayo ni mradi wa maji Dihimba, uzalishaji wa umeme wa viwandani wa megawati 20 katika kijiji cha Hiyari, pamoja na kikundi cha vijana cha utunzaji mazingira — Hiyari Dangote. Mwenge umeridhishwa na utekelezaji wake.

Pia soma Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mwenge wa Uhuru 2025 unatarajiwa kukamilisha mbio zake katika Mkoa wa Mtwara hapo kesho katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Credit Mtwara Online TV
 
Back
Top Bottom