Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

Naunga mkono hoja,lakini pia upangiwe Bajeti yake sio kucha
Bila shaka kichwa cha habari kinajieleza vizuri sana.

Binafsi sina tatizo na falsafa ya uanzishwaji wa mbio za mwenge wa uhuru. Tatizo langu kubwa ni namna wanavyoweza kuathiri afya za wanaoukimbiza.

Nishati inayotumika sio rafiki kwa afya za wanaoukimbiza na hata walio karibu nao mahali unapowasili.

Kama tunavyofanya jitihada za kuzuia matumizi ya kuni na mkaa kwa kupikia, vivyo hivyo tujitahidi kubuni njia mbadala ya kuufanya mwenge wa uhuru uweze kutoa mwanga. Vijana wanateseka sana na moshi.

Naomba kuwasilisha.
View attachment 3058976
Naunga mkono hoja, lakini pia utafutiwe Bajeti yake badala ya kuchangisha Watumishi maskini wa Umma.
 
Kama tunavyofanya jitihada za kuzuia matumizi ya kuni na mkaa kwa kupikia, vivyo hivyo tujitahidi kubuni njia mbadala ya kuufanya mwenge wa uhuru uweze kutoa mwanga. Vijana wanateseka sana na moshi

Miaka tunasoma, ilikuwa kila mwaka kuna shilingi 1 ya mchango wa mafuta ya mwenge...
 
Mwenge una faida gani?
una faida ya kutukumbusha miiko na na maadili yetu kama taifa kwakuwa hautukumbushi tena ni amma tuuzime au turejee maandiko yake. manzie mangochie DC wa zamani wa chatto yupo wapi kwa sasa. huyu aliutumia mwenge kuweka watumishi ndani akijitapa kwamba membe ni raisi ajaye akiwaita wengine marofa.
 
Back
Top Bottom