Mwenge wa Uhuru wafikishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, waimba Wimbo wa Taifa

Hivi hili tukio hufanyika Kila Mwaka ama ni Mwaka huu pekee wameamua kwenda kuzimia Mlima Kilimanjaro?

By the way, Kila la heri Mama Tanzania 👊
Uchochoro wa kuchochora pesa za umma babu😅
 
2024 vijana mnashadadia kukimbiza moto mlimani kweli? Hiyo bajeti si ingeweza kuwasogeza walau mkajemgewa viwanda viwili vitatu kukabiliana na soko la ajira.
 
Wakati wanauimba huo wimbo huku wanaumauma maneno, ndio nami nikakumbuka naelekea kuusahau huu wimbo🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Uchochoro wa kuchochora pesa za umma babu😅
Ila Mwenge haunaga Bajeti isipokuwa michango ya Wadau

Nimechangia sana kupitia eneo langu la biashara

Labda kama inakwepo hapo Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini seems huko Chini haifiki 🙌
 
Hivi hili tukio hufanyika Kila Mwaka ama ni Mwaka huu pekee wameamua kwenda kuzimia Mlima Kilimanjaro?

By the way, Kila la heri Mama Tanzania 👊
Wakifika hapo kileleni walitakiwa wauwashe na siyo kuuzima. Kuzima mwenge kileleni mwa Kilimanjaro kuna maana mbaya katika matambiko ya Kichagga. Ndiyo maana nchi ina gundu haiendelei

Mshana Jr
 
Ina maana gani Mkuu ili tusio wachagga tuelewe, huenda tukapata nafasi ya kushauri mbele ya safari 🙏
 
Kuzima moto katika mila za Wachagga ni kitendo kinachofanyika wakati wa msiba au kifo cha mpendwa. Katika mila hizi, "kuzima moto" kuna maana ya kusitisha au kumaliza shughuli zinazohusiana na maisha ya kawaida ya nyumbani, hasa zile zinazohusiana na kupika au kuwasha moto kwa shughuli za kila siku. Ni ishara ya heshima kwa aliyefariki, na ni sehemu ya kuomboleza kifo cha mtu muhimu katika jamii au familia.

Kuzima moto mara nyingi hufanywa kama sehemu ya taratibu za mazishi na inaashiria kwamba nyumba hiyo imepoteza mmoja wa wapendwa wake, hivyo maisha hayawezi kuendelea kama kawaida hadi taratibu za maombolezo zitakapokamilika. Wakati mwingine, moto unaweza kuwashwa tena baada ya kipindi maalum cha kuomboleza au baada ya ibada za mazishi kukamilika, ishara ya kurudi katika hali ya kawaida ya maisha.

Katika baadhi ya familia za Kichagga, kunaweza kuwa na matendo maalum au ibada zinazohusiana na kuzima moto, na kwa kawaida kitendo hiki hufanywa na mtu wa ukoo au mzee mwenye mamlaka kwenye familia.
 
Au ikiwapendeza wasipeleke kabisa huo mwenge huko kileleni mwa Kilimanjaro
 
Shukrani Kwa Elimu hii Mkuu

Leo nimejifunza jambo jipya kupitia wewe

Barikiwa sana 🙏🙏🙏
 
Wakuu,

Mbio za mwenge zilihitimishwa tar 14, Oktoba na wakimbiza mwenge huo kutakiwa kukamilisha zoezi hilo kwa kufika katika kelele cha mlima huo pamoja na kuweka bendera ya taifa.

Wajuba walikamilisha zoezi na hapa wanaimba wimbo wa taifa kwa uzalendo mkubwa uliotukuka!

Pia soma: Rais Samia akishiriki kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukizi ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere

..upumbavu mtupu.

..inatusaidia nini kupeleka mwenge kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro?

..Ni matumizi mabaya ya kodi.
 
Back
Top Bottom