Mwenge wa uhuru wakagua tanki la maji Buhongwa, wananchi zaidi ya 80,000 kunufaika

Mwenge wa uhuru wakagua tanki la maji Buhongwa, wananchi zaidi ya 80,000 kunufaika

Oneonone

Member
Joined
May 5, 2026
Posts
17
Reaction score
17
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Mwang’onda, ametembelea na kukagua utekelezaji wa Tanki la Kuhifadhia Maji la Buhongwa, jijini Mwanza, na kueleza kuridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi huo unaolenga kuboresha huduma ya maji kwa wananchi zaidi ya 80,000 wa Buhongwa na maeneo ya jirani.

94608919-c381-4d38-9019-deeececddcb8.jpeg

Tanki hilo lenye ujazo wa lita milioni 10 na thamani ya takribani Shilingi bilioni 3.3, limefikia asilimia 85 ya utekelezaji na litasaidia kuhifadhi na kusambaza maji kutoka Chanzo cha Maji cha Butimba kwa wananchi wa Buhongwa, Sahwa, Kanindo, Kagera, Igwambiti, Nyashishi na Nyahingi.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Ndugu Mwang’onda ameipongeza MWAUWASA kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo na kutumia fedha za Serikali kwa lengo lililokusudiwa, huku akiielekeza Mamlaka kuendelea kumsimamia Mkandarasi ili mradi ukamilike kwa wakati na kwa kiwango kinachokubalika.

58d39a1b-c404-4b01-9921-67e56d18d9b2.jpeg

Aidha, amewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya maji kwa kuhakikisha hailindwi tu wakati wa utekelezaji, bali inaendelea kutunzwa ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu.

"Mradi wa Tanki la Buhongwa ni sehemu ya Mradi wa Ujenzi wa Matenki Matano, Ulazaji wa Mabomba Makuu ya Kusafirisha Maji na Vituo Viwili vya Kusukuma Maji, unaotekelezwa kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Victoria kwa gharama ya Shilingi bilioni 46.2 bila VAT. Mradi nahusisha matenki yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 31 pamoja na mabomba makuu yenye urefu wa kilomita 40.5." Ameeleza Mhandisi Nuhu Said Msimamizi wa miradi MWAUWASA

94608919-c381-4d38-9019-deeececddcb8.jpeg

Utakapokamilika, mradi unatarajiwa kuboresha huduma ya maji kwa takribani wananchi 450,000 katika Jiji la Mwanza na maeneo ya pembezoni.

MWAUWASA inaendelea kuhakikisha uwekezaji huu unazalisha matokeo yanayolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, sambamba na kutimiza azma ya Serikali ya kuimarisha huduma za msingi kwa maendeleo ya wananchi.
9ba84d60-ab80-4a9b-af9d-981216b9eca9.jpeg
 
Attachments

  • 8804e6f4-0c51-4183-887f-218d3908f9cd.jpeg
    8804e6f4-0c51-4183-887f-218d3908f9cd.jpeg
    122.6 KB · Views: 15
Moto unakagua tenki?

Kwahiyo bila huo moto tenki lisingekuwepo?

Huu upuuzi utaisha lini , kwani wananchi wasingekabidhiwa tenki kwa matumizi bila kuleta moto maji yasingetoka?
Kwani huo Mwenge wa Uhuru ukikagua wewe unapungukiwa nini?
 
Kwani huo Mwenge wa Uhuru ukikagua wewe unapungukiwa nini?

Mwenge ndio ulileta uhuru?

Hebu nieleze mwenge uliendaje UN kudai uhuru.

Mwenge ukague tenki je huo mwenge una taaluma ya uhandisi au huko kukagua ulimaanisha nini?

Huo moto uitwao mwenge usingepita hapo maji yasingetoka?

Na huo mradi uliogharamiwa na kodi za wananchi wangeweza kupewa tayari kwa matumizi bila kuita moto huo mnaoita mwenge kwa kisingizio umeenda kukagua.

Gharama za msafara wa magari, mafuta, posho kukimbiza huo moto zingeweza kuweza kujenga tenki lingine.
 
Kuna maswali mengine ni upumbavu na hatuyajibu.
 
Mambo ya mwenge yalipitwa na wakati
sijui kwanin huu ujinga wa 1961 upo mpaka leo 2026
ni upotevu wa hela na nguvukazi!
 
Back
Top Bottom