SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Waswahili wanapenda sana kukomalia mambo ma hata pale ushahidi ukiwa hafifu au wakiletewa ushahidi tofauti na wanachotaka kuamini, wanakuwa wagumu kukubali.
Nimeona clip inayosambaa ya basi la Simba likirudi kinyume katika mtaa mmoja mwembamba. Kwanza sielewi kinachoshangaza nini kwa gari kurudi reverse. Niwakumbushe tu hii technology ya reverse imekuwepo kwenye magari kwa miaka mingi sana na inatumika kila siku. Sasa hivi tu unaposoma huu uzi kuna magari mengi tu muda huu yanaenda kinyumenyume. Kingine tena ukiangalia clip hiyo inayosambaa ni katika mtaa ambao ni wazi hilo basi lilikuwa linaenda kugeuza.
Wengine wamediriki kusema hilo basi limeendeshwa hivyo siku ya jana kutokea Bunju hadi Uwanja wa Taifa na kuna watu kabisa wanaamini hivyo.
Sasa ili tukate mzizi wa fitna ili tuachane na hili tuongelee mambo mengine ya maana, embu tumeni clip nyingine ikionyesha basi hilo likipita eneo tofauti na hapo likiwa bado linaendeshwa hivyo au clip ya eneo hilo hilo lakini linapita eneo ambapo lingeweza kugeuza lakini halifanyi hivyo.
UPDATE: Ni wazi hakuna mtu mwenye clip zaidi ya hiyo kwa hiyo hii mada tumeifunga rasmi. Kuna mada za kijinga ukizijadili zinapunguza uwezo wako wa akili.
UPDATE 2:
Video ya Saleh Jembe akitoa maelezo kutoka eneo la tukio.