Miaka michache (chini ya 5) iliyopita, nilikua nahitaji kijana msomi na makini mno ili asimamie biashara yangu mpya. Niliwafanyia interview graduates 32 na sikupata mtu. Mama yangu akaniambia tafuta chuo chochote Dar, ulizia mwalimu wao wa biashara, mwambie nature ya biashara yako, muombe akupe wanafunzi waliomaliza ambao anaona watafaa kwa biashara yako. Alafu muahidi akikupatia mtu sasa, utamlipa laki 2.
Nilifanya hivyo, nikatanguliza 50. Huyo mwalimu alisema anae mtu ila alikua ana mreserve kwa ajili ya project yake mwenyewe. Alinipa namba siku hio hio, nikamfanyia interview kesho yake, na kumpa ajira bila hata kuona hio degee yake. Alikua ni kijana sahihi sana kwa biashara yangu, na yeye nikampa jukumu ya kutafuta wasaidizi wake wa ngazi za chini. Hamna pesa niliyowahi kuitumia vizuri kama hio laki 2 .
Katika hii miaka 10 iliyopita, mie binafsi nimeshawanyia interview vijana zaidi ya 700, nafasi tofauti tofauti, kati ya hao, graduates zaidi ya nusu, na kati ya hao, walioweza kupata ajira, hawazidi 20. Tatizo kubwa ni vijana hawajiongezi, hawaendi the extra mile required, uaminifu ni tatizo kubwa mno, hawasomi vitabu au majarida kuona dunia inaendaje kwa sasa, kuna university of 'utube', ni bureeee ila vijana wako busy kuona diamond kazaa na nani, tako la bby mama wake ni lake au kigodoro, na vyote hivyo vinatumia bando. Ukienda nchi jirani tu hapo, unaweza kua na nafasi 2 ila wanaofaa hio nafasi zaidi ya 15, unachanganyikiwa umuache nani, umchukue nani. Ila hapa nyumbani, kuna tatizo kubwa mno la vijana wetu kwenye issue ya interviews na ajira kwa ujumla.