ndugu mimi nishajaribu hizo dawa siku moja, niliacha siku hiyo hiyo maana niliipiga wakayi sio, yani nimeamka asubuhi nikainywa then nikaingia mishe posta daah kilichonipata nilishikwa na tumbo la kuhara nikiwa kwenye daladala na kila nikisaka choo posta sipati huwezi amini nilikipatia mnazi mmoja, nishakaza misuli mbaya... nikasema sigusi tena, nikajaribu zile diet zao za wiki mbili kilo 10 unapungua ila kabla ya kuanza nikapewa ile diet nikaanza kuhisi njaa pale pale, kwa mwanaume inalegeza sana hizi diet, kuna jamaa angu alipiga diet akapungua kweli kama kilo 13 ndani ya mwezi ila alikua dhaifu kochi kunyanyua hawezi...
nilichoamua ni kufanya mazoezi kila siku na kupunguza mafuta na sukari na kutumia white meat a.k.a protein kwa wingi, kunywa maji mengi, kuacha soda na kupunguza bia sasa hv mpaka wikiendi...
mazoezi nayofanya
1. kuruka kamba
2. pushups 50-80 per day.
3. situps za tumbo 75-100 per day
4. kutumia roller 20 round per day.
5. kuzunguka uwanja 10 rounds per day.
nikitoka hapo nalala murua sana na naona improvements kibao...
ILA ALL IN ALL MAZOEZI YANAHITAJI MOYO SANA KUNA SIKU NATAMANI NISIGUSE ILA NAENDA TU.