Mwenye idea na octopic pregnancy

Mwenye idea na octopic pregnancy

mandingo6262

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
424
Reaction score
81
Jamani naombeni maelezo kidogo kuhusiana na hili, kuna rafiki yangu ni mjamzito ila baada ya kujikuta akisumbuliwa na maumivu ya tumbo alienda hospitali na kupigwa ultra sound walimwambia kuwa mimba imetunga karibu na mrija wa uzazi, cha ajabu ni kwamba ameendelea kuumwa tumbo na kutapika, hana hana hamu ya kula na hospitali walichosema ni kwamba asubiri kama akiona dalili za kutokwa na damu ukeni basi aende hospital. Naombeni mnieleweshe kuhusiana na hili
 
Mmh! Ectopic then wamemwambia asubiri....ninawasiwasi na maelezo ya daktari coz sio lazima mimba zote zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi mgonjwa atoe damu...mwingine damu inavilia ndani ya mfuko wa uzazi na inaweza kuleta complication..

Na anapozidi kukaa mtoto anazidi kukua hali inayohatarisha usalama wa mrija wake wa uzazi..
Japo zipo mimba zilizoanzia ktk ectopic na kujiimplant kwenye mfuko wa uzazi but chance ni ndogo sana so ushauri wangu mimi ni kinga ni bora kuliko tiba asisubiri hali iwe worse...mpe pole sana.
 
Inaonekana daktari anamtisha! Ye aliambiwa kuwa wanadhan mtoto anavyokuwa basi akashuka kwny uterus, bt kama hatashuka inamaana kabla ya wiki 12 itapasuka hivyo atahitaj upasuaji na kutoa mrija. Je ni sahihi asubir had tatizo litokee au madaktar watakuwa wanabahatisha?
Then kuna uwezekano ultra sound kudanganya?
 
Implantation ya mtoto hufanyika ndani ya wk baada ya yai kupevusha mpaka wiki mbili..ckatai maelezo ya daktari wake coz yeye ndo anajua full case ya mgonjwa wake but sioni kama ni sahihi kusubiri mirija ipasuke coz itahitaji operation badaae au inaweza kumcost huyo dada kuwa na mrija mmoja baada ya mwingine kupasuka...bado niko pale pale kuwa kinga ni bora kuliko tiba ...
kuna njia nyingi za kuinduce abortion kwa ctuation kama hiyo kusubiri mtoto akue kunaweza kuleta neg impact..
 
Mmh!hilo ni tatizo kubwa je dk.aliekwambia hivyo ni bingwa wawanawake?,kwani ni hatari sana naupo mkoa gani kama uko arusha kaonane na sweke,selian hosp.aliokoa maisha yangu kwa shida kama iyo,nakushauri uonane na bingwa wa wanawake,
 
Mwambie aende hospital nyingine kwa uchunguzi zaidi kwani nijuavyo mimi ectopic ni hatari kwa maisha ya mama
 
Asanteni kwa ushauri wenu, tatizo ni hizi hospitali zetu za kwenye mikoani, itabid aende kwenye hospital kubwa akutane na gyno.
 
Back
Top Bottom