Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa


Wewe jiulize kwanini mpaka leo hatajwi mwenye jengo?. Lakini kuna wapangaji wa hilo jengo, hivi hawamjui nani mmiliki?
 
Wewe jiulize kwanini mpaka leo hatajwi mwenye jengo?. Lakini kuna wapangaji wa hilo jengo, hivi hawamjui nani mmiliki?
Uchunguzi unafanyika, muda sio mrefu atafikiwa tu na yeye.
 
Yeye hajaiba anavibali halali kabisa vya kuboresha ujenzi hapo.
 
Mmiliki jengo na biashara aliajiri kandarasi ya kupanua eneo kwenye 'basement' kwa kuvunja kuta na kuchimba ndio chanzo cha ghorofa kupiga magoti.

Kibali aliomba kutoka kwa mamlaka husika lakini hawakwenda kutathimini kama uwezekano wa upanuzi huo ulikuwa unawezekana bila kusitisha shughuli zingine za biashara katika jengo hilo, hivyo kuna utata hapo.........

Basement inayojengwa chini ya ardhi ni sharti iwe ni ya mfumo wa kichanja kilichosukwa kwa nondo kuanzia 16mm, 25mm na 45mm na kitanda/kitako cha kulalia uzito lazima kiwe na uwezo wa kunyumbulika.

Hata hivyo kwa tukio la kuanguka ghorofa Kariakoo sababu ni mbili kuu

1. Ramani ya ujenzi na vifaa ni hafifu
2. Kubadilisha ramani ya jengo chini ardhini kwa ajili kupanua maeneo ya kukodisha wafanyabiashara bila kuzingatia kanuni ya uhandisi na usalama

Check out the engineering structural setup
Underground Basement Construction Steps​

It involves digging a large pit in the ground, installing a temporary retaining wall around the perimeter, and then building the basement structure from the bottom up. The soil excavated from the pit can be reused or disposed of, depending on the site conditions and regulations.

  • Excavation: Contractors remove soil, rocks, and debris to create the desired underground space. They may use a backhoe or excavator to dig the pit.
  • Temporary support: Engineers design temporary devices to support the building during construction. Horizontal support prevents the soil from collapsing, while vertical support keeps the building from shifting.
  • Foundation: The engineer designs the foundations, walls, and bases for the basement.
  • Retaining wall: A temporary retaining wall is installed around the perimeter of the pit.
  • Construction: The basement structure is built from the bottom up.
  • Diaphragm walls: A reinforced concrete wall is built deep into the ground to provide structural support and prevent water seepage.
  • Roof slab: The roof slab for the first basement floor is created.
  • Superstructure: Construction of the superstructure begins.
  • Repeat: The process is repeated until the desired depth is reached.
  • Top-down: A technique where reinforced concrete diaphragms are cast in situ, followed by the creation of the roof slab.
  • Double bit: A common arrangement for basement construction.
  • Open-cut: A method that combines open-cut and top-down arrangements
 
Dahihi i
Mwenye jengo pia anahusika. Amefanya kitu hatarishi
La hawa watoa vibali ndio wenye shida ndio root . Mwenye Jengo atafanyaje hivyo bila permit?. Ni sababu ya waroho wachache maisha ya watu yameenda
 
Kama ana vibali halali vya kumiliki na kufanya maboresho aliyokuwa anafanya kama ni kweli, basi hagusiki?
Kingekuwa kipindi cha utawala wa ka Jiwe wala usingesema hivyo! Kwanza sasa hivi angekuwa ameshakamatwa na maafisa waliohusika wangekuwa mikononi mwa Jiwe! Hakika rushwa waliyokula ingewatokea sehemu zote zilizo wazi!
 
Dahihi i

La hawa watoa vibali ndio wenye shida ndio root . Mwenye Jengo atafanyaje hivyo bila permit?. Ni sababu ya waroho wachache maisha ya watu yameenda
Wakamatwe wote na wanyongwe hadi kufa! Kesi yao wala haihitaji kusikilizwa! Ni kukamata na kuhukumu hapo hapo!😁😁
 
Ati mwenye ghorofa akamatwe ebo ! Ninani alitoa kibali Cha kuruhusu jengo lifanye kazi na Hali hata ukiliangalia tu lilikuwa bovu? Ninani huwa anakusanya Kodi?

Mamlaka ya kudhibiti ubora na wakaguzi wote walikuwa wapi? Na sasa yapo mengine nimeyaona yana nyufa na kreki na mengine yameinama kabisa, serikali ikamatwe na iwajibishwe kwa uzembe huu ikiwezekana ihukumiwe kifungo gerezani.
 
Yeye hajaiba anavibali halali kabisa vya kuboresha ujenzi hapo.
Wewe unajuaje kama ana vibali halali vya kuboresha ujenzi?
Kama amehonga ili aboreshe tu bila vibali halali?
 
Wewe umefafanua vizuri na kutoa sababu za kiufundi. Ubarikiwe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…