X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
Ndugu zangu,
Rejea kwenye post yangu NATAFUTA KAZI MAJI YAMENIFIKA SHINGONI.
nafanya kazi kwenye kampuni moja ya ulinzi GARDAWORLD nalipwa 240,000/= kwa mwezi hapo makato yote yamesha katwa. Japo nina diploma ya uandishi wa habari, nimetafuta kazi inayoendana na elimu yangu takribani miaka mitatu bila mafanikio.
Juzi nimeona tangazo la nafasi za kazi tena za ulinzi kwenye hii kampuni yenye jina NGUVU MOJA SECURITY. Kwa anayeifahamu hii kampuni naomba anisaidie sifa zake kwani nafikiria kwenda kupeleka barua zangu za maombi ya nafasi za kazi walizotangaza za ulinzi wa migodi. Sasa naogopa nisije nikaruka mkojo nikaangukia kwenye kinyesi kigumu.
Nahitaji kujua
1. Je, wanajali wafanyakazi wao?
2. Je, wanalipa kiasi gani?
3. Wanazingatia elimu kwenye malipo yao ya mishahara?
4. Kuna marupurupu yoyote mengineyo wanayoyatoa haswa kwa walinzi wa migodini?