Mwenye Kujua Dawa ya Kuangamiza Mende

Mwenye Kujua Dawa ya Kuangamiza Mende

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,176
Enyi matabibu wa JF.

nisaidieni wajameni. natafuta dawa ya mende wananisumbua sana. dawa za kihindi za kupuliza nimejaribu aina aina lakini nimenawa, maana nikiwapuliza wanalala tu badala ya kufa.

Dawa za kupuliza wamezigeuza viroba wanazitamani kweli ili walewe.

Mnaweza kuchukulia utani, ila niko siriaz.

Naomba msaada wenu wa kitabibu.
 
Kaka tafuta dawa ipo kwenye vipakiti vya kijani gram 5 iv. Inaitwa cockroach kiling balt (green leaf) ya unga.

Wanauza machinga, nakuambia ni kiboko sijawai ona ndugu. Inauzwa buku tu.

Mende wote wanapotea kabisa huwezi amini. Wasipo potea naomba uni pm nikurudishie gharama ulizotumia.
 
Green leaf kiboko asikudanganye mtu mim nilizoa mende nusu ndoo had wajukuu wote kushney jaribu hautojuta.
 
Unauliza mende? Nenda chooni.
 
kweli hiyo dawa inaonekana ni kiboko maana hata jamaa yangu kasema vivyohivyo kama wachangiaji hapo juu.
 
Hahaaha,mimecheka mpaka mbavu zimechomoka, dawa washaifanya viroba, du, hii kali
 
Dawa ya kuuliza Mende?

Mkuu hiyo cockroach kiling bait green leaf ni kweli inamaliza kabisa ila zipo mbili kuna fake na Original so ni bora ununue zote moja ina rangi ya dark green na nyingine kidogo ipo right green mimi huwa zinanichanganya japo nilisifiwa kwa Office mwaka 2007 pale nilipodhibiti mande wadogo wadogo wasioisha na nilichukia sana pale dukani mtaa wa Morogoro road kuna ki supa market ndio kilikuwa kimefunguliwa katoka pita pita zangu za procurement nikakutana nacho hicho kitu ila baada ya mwezi mtu akaniuliza nikamuelekeza akaenda akaambiwa zimeisha sikuamini nikaenda mwenyewe wakaniambia wameagiza ila ndio hawakuleta tena walikuja niambia wenzio wananunua maboxi na maboxi nikaanza kuziona mitaani tu fake na original.

 
Kuna dawa moja maarufu inaitwa CHAKAZA...bahati mbaya haipatikani hovyo madukani...but hiyo to me ni the best....nilihamia nyumba yenye vimende wale wadooogo ukifungua kabati wamo,kwenye madroo haoo..ndo nikaweka hiyo dawa..nina mwaka wa pili sasa sijaona mende akikatisha katika himaya yangu.
 
kuna dawa moja maarufu inaitwa CHAKAZA...bahati mbaya haipatikani hovyo madukani...but hiyo to me ni the best....nilihamia nyumba yenye vimende wale wadooogo ukifungua kabati wamo,kwenye madroo haoo..ndo nikaweka hiyo dawa..nina mwaka wa pili sasa sijaona mende akikatisha katika himaya yangu

Hii ni kweli kabisa hata mimi nilitumia dawa hiyo tangia wiki mbili hivi kwa kweli wamepotea kabisa mpaka najiuliza wameishia wapi? Maana ilikuwa ukiamka usiku unakuta wanacheza "brake dance" kila mahali na wakati mwingine hata mchana hasa kukiwa na wageni.

Niliinunua kariakoo floor ya kwanza pale palipokuwa corridor enzi hizo nakuja mjini (1947) ingawa sasa wamepageuza viduka vidogo vidogo. Nilikuta kimebaki kichupa kimoja siku ile ila kimefanya kazi ya ajabu. Ni dawa unachanganya na maziwa halafu unaweka sehemu wapitazo>

Mleta hoja aliposema kuwa za kupuliza wamezigeuza kituko ni kweli kabisa labda sababu ya kuchakachua kwani hata kwangu ilikuwa hivyo hivyo, kuna siku nilikuwa niwe na wageni nikapuliza nyumba nzima jana yake lakini ilikuwa kama nimewachokoza kwani walifanya fujo za kutosha tu mbele ya wageni mpaka nikajuta kwa nini nilipuliza dawa hiyo.

Halafu ukikosa Kariakoo waweza ni PM ili jioni nikutumie namba ya wazalishaji kwani imeandikwa kwenye kichupa hicho
 
Hii ni kweli kabisa hata mimi nilitumia dawa hiyo tangia wiki mbili hivi kwa kweli wamepotea kabisa mpaka najiuliza wameishia wapi? Maana ilikuwa ukiamka usiku unakuta wanacheza "brake dance" kila mahali na wakati mwingine hata mchana hasa kukiwa na wageni...

kweli kaka unaijua ni kweli unamix na maziwa but its the best dawa ever....yssni wanmgeweza wangenipa umarketing Manager maana nimeelekeza watu kibao..nao wote wameprove kwamba ni the best
 
Sio kweli. Kwenye makaro ya chooni yale mavi utamaintain vp usafi bila kutumia madawa?

Mende wanaweza anzia kwako au kwa jirani.

Mende wale wakubwa wa chooni. Dawa yao ni hii: Nunua vidinge 4 vile vya Ngao ya kuulia mbu, kisha changanya na maji ndoo moja. Kisha yamwage chooni. Mende kwisha habari yao.
 
Ukishindwa hizo walizo kueleza. Jaribu kutumia Dip. Nayo inafaa kwa kuwa wadudu.
 
Kaka dawa ya mende usafi tafuta wkend moja fanya usafi wa nguvu ukitumia mafutaa na sabini za maji au unga kwenye maficho yao toa kila kitu nje anika juani kwa masaa manne matano hv rudisha ndani panga upya.angalia kama una housegal asiwe anabakisha na kumwagamwaga vyakula usafi upewe kipaumbele mimi nimewadhibiti kwa jinsi hii
 
Mende ni wadudu hatari sana kwa afya inahitajika kufanya fummigation usafi hauwezi kumaliza vyanzo na mazalia kwa sasa inahitajika kufanya fumigation kuangalia kabisa Mende hao alafu usafi uzingatiwe isitokee tena pamoja na kupiga dawa baadae ya angalau kila baada ya miezi mitatu kwa huduma Nzuri na nafuu ya fummigation wasiliana nasi 0657835309 tutakusaidia
 
Back
Top Bottom