Mwenye kujua, nje ya Medical Doctor (MD), course gani nyingine ipo kwenye soko miaka 3 hadi 4 ijayo?

Mwenye kujua, nje ya Medical Doctor (MD), course gani nyingine ipo kwenye soko miaka 3 hadi 4 ijayo?

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Habari za uzima, Ndugu zangu, kuna mtoto wa dada yangu nimemfanyia application ndoto zake kubwa ni kusoma udaktari na aya ndio matokeo yake ya O-LEVEL (NI BINTI)

O LEVEL
Civics..........B
History.......D
Geograph..B
Kiswahili....B+
English.......B+
Physics.......C
Chemistry...C
Biology.......B
Basic Mathematics....C

Amesoma Diploma ya Clinical Medicine amepata GPA ya 4.1/5.0

Na vyuo nilivyomfanyia application mpaka sasa ni vyuo 5, (UDOM (MD), UDSM(MD), MUHAS (MD), KCMC (MD), NA ST FRSNCIS CHA MOROGORO (MD) ),

Matokeo yameshatoka ya vyuo vyote nilivyomuombea hapo juu, na mpaka sasa hajapata chuo chochote kile, tangu jana amekaa ndani analia tu, nimejaribu kumuuliza je kuna course nyingine yeyote ya mambo yanayohusina na afya anapenda tuombe yeye anasema yeye alifikili atapata MD, hizo zingine hazifahamu vizuri, sasa naombeni msaada wenu wakuu ni course gani nzuri ambayo ipo kwenye soko la ajira kwa miaka 3 au 4 mbele atakapomaliza masomo yake.

Nawakaribisha kwa ushauri ndugu zangu tumsaidie mdogo wetu.

karibuni.
 
Uwepo wa vyuo vingi vya kati vya binafsi kiujumla unachochea wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kufanya MD. Wanafunzi ‘Wanapewa’ na sio kuihangaikia GPA. Kwa kipindi kile GPA ya 4.1 ni aghalabu kukosa chuo.

Asikate tamaa,ajaribu kuomba kwenye duru la 2 na mungu atamsaidia atapata tu.
 
Habari za uzima, Ndugu zangu, kuna mtoto wa dada yangu nimemfanyia application ndoto zake kubwa ni kusoma udaktari na aya ndio matokeo yake ya O-LEVEL (NI BINTI)

O LEVEL
Civics..........B..
Naishia kusema tu safari hii kazi tunayo huko vyuoni!, yan mwamba katoboa fresh af kakosa vyuo vyote! Aisee hii hatari sana!
 
Uwepo wa vyuo vingi vya kati vya binafsi kiujumla unachochea wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kufanya MD. Wanafunzi ‘Wanapewa’ na sio kuihangaikia GPA. Kwa kipindi kile GPA ya 4.1 ni aghalabu kukosa chuo.

Asikate tamaa,ajaribu kuomba kwenye duru la 2 na mungu atamsaidia atapata tu.
Ila GPA hii ya NNE kapatia nacte nadhani bado kijna amejitahidi sidhani kama ni ya kupewa
 
Ajarbu tu ku reapply atapata nafasi nying zimejazwa na waliopata multiple ko waki confirm chance zitabaki na mostly kaekwa akiba et ko wata Mconsider mungu atamsaidia atimizie ndoto yake! Me piah na one yangu ya 6 hapa kuna course sjachaguliwa!
shukrani mkuu ubarikiwe
 
Uwepo wa vyuo vingi vya kati vya binafsi kiujumla unachochea wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kufanya MD.
Wanafunzi ‘Wanapewa’ na sio kuihangaikia GPA.
Kwa kipindi kile GPA ya 4.1 ni aghalabu kukosa chuo.

Asikate tamaa,ajaribu kuomba kwenye duru la 2 na mungu atamsaidia atapata tu.
sawa mkuu, shukrani
 
Ila GPA hii ya NNE kapatia nacte nadhani bado kijna amejitahidi sidhani kama ni ya kupewa
Nipo kwenye hii field mkuu..! Najua nnachokiongea..! NACTE wanatoa transcript kutokana na matokeo yaliyopelekwa na chuo husika..!

Nakupa assignment, fuatilia CO waliohitimu before 2015 na kuanzia 2015 halafu utapata majibu..!

Baada ya TCU kupandisha GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 kumekuwa na ongezeko kubwa la GPA > 4
 
Duuh basi mtihani
Nipo kwenye hii field mkuu..! Najua nnachokiongea..! NACTE wanatoa transcript kutokana na matokeo yaliyopelekwa na chuo husika..!

Nakupa assignment, fuatilia CO waliohitimu before 2015 na kuanzia 2015 halafu utapata majibu..!

Baada ya TCU kupandisha GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 kumekuwa na ongezeko kubwa la GPA > 4
 
Ajarbu tu ku reapply atapata nafasi nying zimejazwa na waliopata multiple ko waki confirm chance zitabaki na mostly kaekwa akiba et ko wata Mconsider mungu atamsaidia atimizie ndoto yake! Me piah na one yangu ya 6 hapa kuna course sjachaguliwa!
Afate huu ushauri, mfano MUHAS 90 ni multiple selection, wakiachia nafasi atapata tu
 
Afate huu ushauri, mfano MUHAS 90 ni multiple selection, wakiachia nafasi atapata tu
Kwa MUHAS ngumu kiongozi. Wao mara nyingi wanachukua GPA kuanzia 4.4..! Aombe vya private ndo ana nafasi kubwa ya kupata.
 
Habari za uzima, Ndugu zangu, kuna mtoto wa dada yangu nimemfanyia application ndoto zake kubwa ni kusoma udaktari na aya ndio matokeo yake ya O-LEVEL (NI BINTI)

O LEVEL
Civics..........B
History.......D....
Pole kwa mdogo wetu, mpe moyo na umu encourage. Dogo inaonekana ana akili sana, maana ufaulu wake ni mzuri sana, ila itakua wamemnyanyapaa kwa vile hajapita A level, hivyo vyuo alivyoomba kwa kozi ya MD wana tabia ya kutopenda kuchagua ambao hawajapita A level. Ila ASIKATE TAMAA, dogo ni kichwa sana.

Pia, bongo shida sana. Udaktari ukl overated sana bongo, kiasi kwamba kada zingine za afya which are equally important (or even more important i can say) zinakua under rated na kusahaulika kabisa. Sasa hivi kuna baadhi ya kada za afya wako wachache mno kuliko hata madaktari kwa sababu ya kasumba hii. Anyways.

Nashauri aangalie kozi zifuatazo atakavyofanya application duru la pili ambazo pia ni za afya na ni kozi nzuri sana in terms of market na hata kujiajiri pia.

1. BSc Microbiology-Hii inapatikana UDSM anakua mtaalamu wa vijidudu vinavyosababisha magonjwa... Anaweza kufanya kazi mahospitalini, kwenye diagnostic facilities kama LANCET, kwenye taasisi za utafiti, kwenye NGO mbalimbali za afya, viwanda vya dawa, Viwanda vya vyakula na vinywaji (eg Coca cola, TBL, etc) na kwenye taasisi za elimu ya juu kama vyuo vikuu. Pia, ataweza kufungua maabara binafsi ya kufanya uchunguzi wa kimaabara au diagnostic facility.

2.BMLS Microbiology and Immunology- Hii inapatikana MUHAS, inafanana sana na hiyo hapo juu ila yenyewe ni wide zaidi na ina uwanja mpana zaidi na ina component kubwa zaidi ya masuala ya utabibu (Clinical), ina uwanja mpana wa hapo kwenye "Immunology", ikimpendeza baadae anaweza kuja kusoma zaidi hilo eneo la Immunology mfano Masters ya Immunology na akawa mtaalamu wa mfumo wa kinga (aimmune system) na kubobea kwenye masuala ya utafiti, na kutafuta matibabu ya matatizo mbalimbali ya immune system.

3.Bachelor of Health Laborarory Science-Hii inapatikana KCMUCo Ni kozi nzuri kwa maana ya kwamba hawa jamaa wako wachache sana nchini kwetu... Hawa ndio wataalamu wa maabara na sehemu za ajira ni hospitali (kwenye maabara), kwenye taasisi za utafiti, kwenye diagnostic centers kama LANCET, pia kwenye NGO zinazo deal na masuala ya afya na tafiti za afya kama vile HIV, Malaria, Usugu wa madawa, etc. Pia anaweza kujiajiri kwa kufungua maabara yake. Kuna jamaa zangu watatu wamesoma hii, tupo nao kwenye miradi ya HIV huku tunakula hela za Mmarekani.

4.BSc in Molecular Biology and Biotechnology, UDSM
Hii kozi ni tamu sana, na inapatikana UDSM kuna jamaa yangu tulipiga nae PCB akaenda kusoma hii makitu UDSM, sasa hivi anapiga pesa za wazungu tuu, anaweza kufanya kazi kama Laboratory Technician in Industrial and Government Agencies like TFDA, kwa mkemia mkuu wa serikali, NIMR. Au akawa kwenye Pharmaceuticals and Medical Supplies organizations, NGOs za masuala ya afya.

5.Bachelor of Science in Biotechnology and Laboratory Science (SUA)- Hii haitofautiani na namba 4 hapo juu, yenyewe inapatikana SUA.

Hope you find this helpful.
kikoozi
 
Nipo kwenye hii field mkuu..! Najua nnachokiongea..! NACTE wanatoa transcript kutokana na matokeo yaliyopelekwa na chuo husika..!

Nakupa assignment, fuatilia CO waliohitimu before 2015 na kuanzia 2015 halafu utapata majibu..!

Baada ya TCU kupandisha GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 kumekuwa na ongezeko kubwa la GPA > 4
Hii inawezekana kuwa sababu ? Maana naona kuna mabadiliko makubwa sana
 
Pole kwa mdogo wetu, mpe moyo na umu encourage. Dogo inaonekana ana akili sana, maana ufaulu wake ni mzuri sana, ila itakua wamemnyanyapaa kwa vile hajapita A level, hivyo vyuo alivyoomba kwa kozi ya MD wana tabia ya kutopenda kuchagua ambao hawajapita A level. Ila ASIKATE TAMAA, dogo ni kichwa sana...
Mkuu umenipa mwanga mkubwa sana ambao nilikuwa nahuitaji, ubarikiwe mnoo mnoo mnoo
 
Habari za uzima, Ndugu zangu, kuna mtoto wa dada yangu nimemfanyia application ndoto zake kubwa ni kusoma udaktari na aya ndio matokeo yake ya O-LEVEL (NI BINTI)

O LEVEL
Civics..........B
History.......D
Geograph..B.....
Aombe round ya 2, na akikosa MD mwambie aangalie pharmacy, dentist ya pale muhas pamoja na udaktari wa viungo pale kcmc...
 
Pole kwa mdogo wetu, mpe moyo na umu encourage. Dogo inaonekana ana akili sana, maana ufaulu wake ni mzuri sana, ila itakua wamemnyanyapaa kwa vile hajapita A level, hivyo vyuo alivyoomba kwa kozi ya MD wana tabia ya kutopenda kuchagua ambao hawajapita A level. Ila ASIKATE TAMAA, dogo ni kichwa sana....
Hongera kwa kumpa mwanga. Ila vigezo vya sasa vitamkataa, uwanja wa chaguzi ya kozi umepunguzwa. TCU wanataka ufanye chaguzi kutokana na ulichokihitimu kwenye ngazi ya stashahada.

Mfano; Clinical Medicine ni MD, HIS,HMS, Clinical Nutrition na Nutrition Science huruhusiwi kuomba Maabara au Famasi. Na mtu aliehitimu stashahada ya Famasi au Maabara hawezi kuomba MD.
 
Pole kwa mdogo wetu, mpe moyo na umu encourage. Dogo inaonekana ana akili sana, maana ufaulu wake ni mzuri sana, ila itakua wamemnyanyapaa kwa vile hajapita A level, hivyo vyuo alivyoomba kwa kozi ya MD wana tabia ya kutopenda kuchagua ambao hawajapita A level. Ila ASIKATE TAMAA, dogo ni kichwa sana....
Umemshauri vema ila kuna kozi hapo Clinical Medicine hawachukui
 
Back
Top Bottom