kuanzia 2010 watu wengi waliona kupitia route ya diploma ni rahisi zaidi kufikia ndoto zako kuliko form 6. Mtu anamaliza diploma 2020 na kujiunga digrii 2020 yaani ile diploma yake haitumii hata kidogo.
kwa experience yangu wakufunzi wengi hawapendi wanafunzi wanaotoka diploma maana wanaona wanatumia nguvu kubwa kuwaelekeza vitu vidogo. Mtu hana knowledge Nzuri ya cytology, hajui biochemistry ile rahisi ya advance, ana DNA concept ya Olevel. Au mtu anaenda kusoma Bpharm hajui organic chemistry na physical chemistry zile konki za Advance, hajui differentiation na integration wakati zinahitajika kusoma pharmacokinetics na pharmaceutical technology( production)
Sisemi kama ni magumu sana na hawataelewa, wapo diploma holders ambao wanaperform vizuri kuliko form 6 ila the odds are against them na inabidi wastruggle mara 2 ya form 6 ili kuwa level moja. Wakufunzi hasa vyuo vya serikali hawataki shida za kurudiarudia mambo ndio maana wanapenda form 6 ambao wana background nzuri ya hayo mambo.