Mwenye kumfahamu Will Gamba

Mwenye kumfahamu Will Gamba

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Habari,

Mimi nilisoma vitabu vya mwandishi will Gamba wakati nimeanza kujua kusoma has nikiwa darasa la tatu na nne.Ningependa kufahamu kama kuna mwenye taarifa za huyu mtu.Je huyu Will Gamba alikuwa muhusika mkuu kwenye vitabu au alikuwa ndio mwandishi?Wapi naweza pata vitabu vya huyu bwana?Kuna mwenye picha zake atuwekee na mwenye kujua historia yake?

Asanteni
 
Umeshakosea hapo kwa kusema umesoma kitabu cha Muandishi Willy Gamba.

Willy Gamba ni Muhusika Mkuu kwenye simulizi, hivyo kama kweli umesoma sidhani kama ungechanganya.
 
vitabu kama; njama, hofu, kikosi cha kisasi, kikomo, kufa na kupona, na uchu unaweza kuvipata kwa wauzaji posta mpya lakini pia mnazi mmoja pale stand kuna jamaa wanauza hivyo vitabu.
 
Umeshakosea hapo kwa kusema umesoma kitabu cha Muandishi Will Gamba.

Willy Gamba ni Muhusika Mkuu kwenye simulizi, hivyo kama kweli umesoma sidhani kama ungechanganya.
NIlikisoma tena nikiwa darasa la tatu nakumbuka sana kulikuwa na dada mmoja alikuwa anatembeza mkono mbaya na pia nakumbuka majina kama swapo,frelimo na monrovia niliyasikia humo.Natamani nipate nakala nikisoma sisi nikiwa na uwezo wangu wa fikra nilio nao sasa kwakipindi kile kidogo sikumbuki vingi.Vinapatikana wapi?
 
vitabu kama; njama, hofu, kikosi cha kisasi, kikomo, kufa na kupona, na uchu unaweza kuvipata kwa wauzaji posta mpya lakini pia mnazi mmoja pale stand kuna jamaa wanauza hivyo vitabu.
Asante nitatembea huko kupata taarifa na nakala nikajisomeee
 
NIlikisoma tena nikiwa darasa la tatu nakumbuka sana kulikuwa na dada mmoja alikuwa anatembeza mkono mbaya na pia nakumbuka majina kama swapo,frelimo na monrovia niliyasikia humo.Natamani nipate nakala nikisoma sisi nikiwa na uwezo wangu wa fikra nilio nao sasa kwakipindi kile kidogo sikumbuki vingi.Vinapatikana wapi?
Hebu tembelea maduka makubwa/makongwe ya vitabu.

Kwa Arusha hebu tembelea Kase book shop.
 
Hichi kitabu nilisoma nikiwa darasa la tatu, hapo nilikuwa nishaanza kujua kusoma..
Badae nilijikuta nataman sana kuwa mpelelezi, tangu hapo kila nikiulizwa unapenda nn nasema kuwa mpelelezi. .
Willy Gamba alini inspire kiukweli, na hakuna kitabunkigimu kutoka kichwan mwangu kama cha huyu jamaa
 
kweli kabisa hata mimi nilisoma nikiwa darasa la tatu
 
Niko Dar es salaama nafikiria kwenda huko kesho
Kila la kheri.

Kase wapo pale Clock tower...ni Wakongwe sana, hata kama hawana wanaweza kukuelekeza/kukushauri kwa kukipata.
 
Mwandishi huyu alibobea kwenye uandishi wa riwaya za upelelezi. Kama kuna ambaye hajasoma vitabu hivi avitafute asome. Tusibaki tu kuangalia movie kwenye screen kusoma nako kuna uhondo wake wa kipekee.
 
Back
Top Bottom