Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ukiona unampenda mtu halafu bado kuna mambo ambayo unaona unataka uyabadilishe kwa mtu huyo basi tambua hujampenda kwa jinsi alivyo.
Mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu kwa jinsi alivyo pamoja na mapungufu yake,hapo ndio utakuwa umempenda kweli,na hautakuja kuumia kwakuwa umeridhia kwa jinsi alivyo.
Watu wengi huwa wanaona kabisa huyu mtu nampenda,lakini kuna jambo fulani silipendi kuhusu yeye na bado ana matumaini kwamba hiyo kasoro atairekebisha. Iko hivi mtu huwa anaamua kubadilika mwenyewe na sio kwamba wewe unambadilisha,matokeo yake asipo badilika unaanza kulialia. Lau kwamba ungempenda kwa mapungufu yake ungeacha kulia na kuepukana na huzuni zisizo za msingi.
Tumeona mifano kadhaa,watu toka awali wameona wapenzi wao,wana viashiria vya umalaya lakini anajipa moyo kwamba,huyu nikisha muweka ndani nitamtuliza,lakini mwisho wa siku umalaya uko pale pale,lau ungekubali kuwa nae kwa tabia hiyo leo usingelia,maana yake ni kwamba kama tabia fulani huipendi kwa mtu basi mapema sana,jiweke mbali naye la sivyo utaanza huyu mpenzi hanisikii,kumbe umejitakia mwenyewe hayo masahibu.
Weka akilini kwako kwamba,hutaweza mbadilisha mtu labda aamue mwenyewe,kwahiyo usijipe moyo kwamba leo ukubali kuwa na mtu pamoja na mapungufu yake kwa matumaini kwamba eti utambadilisha,hiyo ni asilimia ndogo,kwahiyo kabla hujafika mbali na huyo mtu wako,jiulize je,nampenda kama alivyo na tabia zake?
Usiseme hatuku kwambia
Ni hayo tu!