Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,142
Padri Lucas Mahogha wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge ambaye ni mtunzi wa wimbo wa Nimekukimbilia Bwana Nisiabikie Milele... mwaka huu anatimiza miaka 40 ya upadre. Katika mengi anayokumbuka katika utume wake, mojawapo ni siku moja akiwa katika Parokia ya Biro, katekista wake, Mhuvile alimletea mwanaye ambatize. Akaamua kumpa huyo mtoto jina la Lucas yaani awe somo wake, akambatiza kwa jina la Lucas.
Hata hivyo, baadaye walipoteana na kwa kipindi chote hicho, amekuwa akimtafuta bila mafanikio. Wakati anajiandaa na sherehe ya miaka 40 ya upadre, akashangaa kusikia kwamba mtoto huyo yupo Dara lakini siku hizi haitwi tena Lucas, bali Joti. Anatamani tarehe 31/08/2018 atakapokuwa anatimiza miaka yake hiyo katika upadre, somo wake Lucas awepo.
Tafadhali mwenye namba ya Joti amwambie kwamba anatafutwa na somo wake huko Mahenge.