Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 13,075
- 38,625
Mleta mada pole sana , ndio neno la faraja tunaweza kitamka.
Mleta mada wakati si wa milele, leo unapita njia hii kesho na zinazofuatia kuna njia zake, mabonde milima na tambarare ni sehemu ya hio njia.
Maisha hayawahi kueleweka kwa ukamilifu nini haswa maana yake, ila tafsiri yenye mantiki ya maana ya maisha ni maisha ni mateso na jinsi unavyo fanikiwa kuondoa hayo mateso ndio dhima ya maisha kwa ujumla wake.
Hali unayo pitia binafsi naipitia kupitia mtoto wangu, amekosa usikivu hali inayo mpelekea maisha kuto kuwa kaida.
Yeye kama mtoto anaona kawaida ila mimi mzazi maumivu ninayo yapata haya elezeki!
Baada ya njia za kibinadamu kushibdikana na hata kabla yake nimeendelea kumshukuru mwenyezi Mungu maana makusudi yake hamna anaye weza kuyafahamu.
Hivyo kushukuru kwa hali yoyote kuna leta ssna faraja imani na matumaini..
Pole tena mwenyezi Mungu mwenye huruma na upendo awe nawe kila wakati.