Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lamba unga huoHabarini ndugu wanaJF,
Baba mwenye nyumba amemleta mganga kutoka kusini huko anadai kwenye nyumba yake kuna mtu anamchezea (mambo ya kichawi), sasa anatulazimisha tulambe ungaunga mweupe nimesikia wanauita 'usembe' ili kumbaini mchawi kwenye nyumba yake.
Binafsi nilikataa kulamba vitu visivyoeleweka na sina hizo imani, ila alinichimba mkwala hadi jtano nimpe jibu nikishindwa nihame kwake.
Dhumuni la kuleta hili jambo kwenu mnipe ushauri wa kufanya sababu alinipa siku tatu ambayo ya mwisho ndio leo na hapa nipo job nafikiria nikirudi home nimpe jibu gani.
Kwa kuongezea tumebaki wapangaji wawili ambao tumekataa kulamba hayo madude yake.
Je, yana madhara yoyote kiafya wataalam wa mambo?
Nenda serikali za mitaa then akuandikie notes na serikali z mita wakiwa mashahidi na kama kakutishia pia mripoti mpaka polisi ukae na rb ili aambiwe kabisa usalama wako uko mikononi mwake. then muda ukiisha ndo uhame asikutishe kibwege..kuhama wewe hama tu kwani hiyo nyumba ya kwako? Au ikiungua utabaki hapo? Sema asikutoe ghafla tu wakat hujajipangaHabarini ndugu wanaJF,
Baba mwenye nyumba amemleta mganga kutoka kusini huko anadai kwenye nyumba yake kuna mtu anamchezea (mambo ya kichawi), sasa anatulazimisha tulambe ungaunga mweupe nimesikia wanauita 'usembe' ili kumbaini mchawi kwenye nyumba yake.
Binafsi nilikataa kulamba vitu visivyoeleweka na sina hizo imani, ila alinichimba mkwala hadi jtano nimpe jibu nikishindwa nihame kwake.
Dhumuni la kuleta hili jambo kwenu mnipe ushauri wa kufanya sababu alinipa siku tatu ambayo ya mwisho ndio leo na hapa nipo job nafikiria nikirudi home nimpe jibu gani.
Kwa kuongezea tumebaki wapangaji wawili ambao tumekataa kulamba hayo madude yake.
Je, yana madhara yoyote kiafya wataalam wa mambo?
Angalia usije rambishwa unga wa ngada nawe ukawa teja la Baba mwenye Nyumba, maana siku hizi kuna njia nyingi sana za kufanya watu wawe mateja wa ngada!!sio uswahilini sana ila mwenye nyumba ndio anamambo ya uswahili