Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Mwaka 2015 Mh. Magufuli alikuwa anaomba uongozi wa nchi kwa mara ya kwanza. Alikuwa Bandidu hasa na style ya push ups kuonesha kuwa yuko imara kiafya kuliko mpinzani wake mkubwa Eddo Lowassa ambaye afya ilitetereka kipindi hicho.
Waafrika tunategemea mwanaume anapokwenda kuposa mara ya kwanza anakuwa mnyenyekevu na ndo siku hizi tunawaona wengine wanapiga magoti kuwavika Pete wachumba wao. Lakini kwa Magufuli aliamini atapata tu tena kwa kuonesha "maguvu" jukwaani kwa kupiga push ups na Mapanga Shaaa ya Wanaume Temeke. Alikuwa kibri na mwenye kauli zilizosimama kimamlaka japo alikuwa hajapata mamlaka hayo.
Leo mamlaka anayo maana Katiba yetu yenye viraka na matobo inaendelea kumpa kofia 2 kwa wakati mmoja, Lakini ghafla tumemuona majukwaani si Mara moja kapiga magoti anaomba kura kwa unyenyekevu ambao tunaambiwa kwa wapambe wake anao lakini yeye anakataa na kusema ni Jiwe.
Sasa kama ni tabia yake siku zote, naomba aliye na picha yake ya 2015 akiwa amepiga magoti jukwaani kama alivyofanya juzi Kawe, Wiki iliyopita Njombe nk aniwekee hapa!