Mwenye siti ya dirishani ndani ya basi ana haki zipi?

Ipo hivi ndugu Mtanzania.

(Msafiri kafiri) abilia aliyekata upande wa dirishani hana mamlaka na dirisha ila ana mamlaka na 💺 aliyokalia pamoja na kufungua kufanya anachotaka pasipo kukushirikisha wewe wa pembeni.

Ila ikitokea ukawa na matumizi ya dirisha sababu yupo eneo linalomuhusu, unaweza kumshirikisha sababu ya kero unazoweza kumpa huyo wa upande wa dirishani.

Hakupaswa kufanya huo utoto alioufanya, binafsi huwa supendi kukaa upande wa dirishani but first of all abilia anayekuja nampa sharti la dirisha.

Huyo binti hajakutana na wababe wewe, asee humo kwenye basi siku hiyo wote mlikuwa wenye wokovu mnamsubiri bwana kwa kuepuka 'z'ambi 😄!.
Kweli aisee huyo dem hakukutana na washari wenzie, kuna viumbe wanapenda ugomvi hatari.
Kuna mjomba wangu naona kabisa hilo zogo angelinunua yeye.
 
kisanga cha pili ilikuwa kwenye basi la mkoa tunatoka skul tunaenda likizo.., mzee mmoja alinichomoa siti ya dirishan akadai ni siti yake nkaona isiwe tabu nikatoka nikakaa sit ya kat (3x2)..,sasa siti za mbele kuna mwanafunz mwenzetu alikuwa anaumwa na yeye alikaa sit ya dirishan. Jamaa akawa anajiskia kutapka akaambiwa afungue dirisha tapike nje daah..., ile anatapika yale matapishi nusu yalifanikiwa kwenda nje na nusu yalirudi ndan kutokana na upepo mkali..sasa yule mzee alioga matapishi 70% na 30% yalitufikia sisi wengine. Asee mzee alifoka sana ila me nlikuwa nacheka internally...
 
Wakuu,

Unaweza kuona kama swali dogo hivi ila ni la msingi sana,kama hujakutana na mgogoro wake basi kuna siku utakukumba tu [emoji3]

Siku kadhaa zilizopita nilipanda basi kwenda mahali fulani,kilichofanya niulize swali ni tukio hili;

Upande wa kushoto dirishani alikaa Mdada umri wa kati tu(25-30).Mimi nilikaa siti ya za upande wa kulia lakini ni kama tulikuwa usawa mmoja tu.

Gari ilianza kuondoka bila shida,tatizo lilianza baada kama ya saa mmoja hivi spidi ikiwa kali ndipo yule dada akafungua dirisha lake ili hewa iingie kwa ajili yake,sasa mara baada ya kufungua haikupita hata dakika moja zikaanza kelele kutoka nyuma yake(siti za nyuma yake na zingine za upande wangu) zikimtaka afunge kioo, alisikia lakini hakufunga,baada ya muda mfupi mmoja wa wanaume waliokuwa siti ya nyuma akafunga kile kioo, Yule Dada akafungua tena,hapo akaambiwa "wewe dada funga hilo dirisha upepo ni mkali sana kuna watoto huku nyuma" yule dada akajibu hata mimi najisikia vibaya nahitaji hewa iingie.

Mzee mmoja wa siti ya nyuma akalifunga lile dirisha kwa nguvu aliporudisha tu mkono dada akafungua tena,mzee akafunga dada akafungua tena huku wale waliokuwa wakilalamika nyuma wakishuhudia[emoji3][emoji28],hapo ikainuka vita Kali balaa kelele za nyuma zikazidi kumshambulia yule dada"huyu dada hana adabu kabisa tunawambia haelewi,kuna watu wana watoto wa miezi sita huku nyuma upepo mkali sana,yule dada akajibu namimi najisikia vibaya kwahio nifanyeje?

Kelele zilipozidi akaja konda wa kwanza"Dada funga hilo dirisha huwezi kusumbua watu wote hawa mtu mmoja"alikuwa anaongea huku anafunga hilo dirisha, (kwa maoni yangu huyu konda alikosa busara)dada akamjibu mimi najisikia vibaya nahitaji hewa ndio maana nimefungua,alipoondoka Konda kuelekea nyuma yule dada akafungua tena dirisha.

Yule konda aliporudi kutoka nyuma akakuta dirisha limefunguliwa tena"we dada naona ni mkorofi tutakushusha"dada akamjibu sawa nishusheni ila mnirudishie nauli yangu yote.

Kelele za kumtaka afunge dirisha hazikwisha, huku wale kinamama wenye vichanga wakimshambulia"wewe hujawahi kuzaa ndio maana huna huruma, huyu hana mtoto ndio maana mjeuri"yule dada akajibu nimeshazaa ila namimi nina matatizo ndio maana nimefungua dirisha.

Kelele zilipozidi akaja konda mwingine (kwa maoni yangu huyu ana busara) akawambia dada ukifungua dirisha lako upepo unawaathiri zaidi walionyuma yako kwahio kama unashida ya hewa naomba nikuhamishie siti nyingine ambayo utaweza kufungua,kule nyuma kuna vichanga"

Siku sikia alijibu nini ila nadhani dada aligoma pia kuhamishwa yule konda akamwacha akaondoka zake.

Basi zoezi la mzee wa siti ya nyuma kufunga na dada kufungua likaendelea baadae mzee akachoka ikabidi aache tu ila lawama za wale kinamama zinaendelea pamoja na wale wanaume wa nyuma(hawa wote lilikuwa lile kabila fulani kubwa kanda ya ziwa) basi wakawa wanasapotiana na kumshutumu yule dada kwa maneno mbalimbali baadae kukawa kimya huku dirisha likiwa wazi mpak mimi niliposhuka kituo fulani nadhani na yule dada alishuka pia pale.

Sasa nauliza wadau,hivi haki za mtu mwenye siti za dirishani ni zipi?Je huyo dada alikuwa sahihi au alikosea?Je ni mhudumu ndio anapaswa kufungua ili kuepusha migigoro kama hii?

Karibu.
bandiko lako ni fikirishi SanÄ…...duh
 
Andiko zuri sana na lenye kubungua bongo.
Ni kweli watoto wanasumbuliwa sana na baridi.
Vile vile kuna watu wazima wana shida ya upumuaji.
Hewa ikipungua wanahangaika sana.
Ninaye ndugu yangu ambaye asipopata kiti dirishani yuko radhi kutosafiri.
Wengine.hutapika sana.

Si ajabu kuwa binti huyu alikata tiketi siku kadhaa kabla ya safari ili apate kiti cha dirishani.

Ni changamoto kubwa.
Huenda ndiyo sababu konda "kwenye busara" aliondoka kimya kimya.
 
Kweli aisee huyo dem hakukutana na washari wenzie, kuna viumbe wanapenda ugomvi hatari.
Kuna mjomba wangu naona kabisa hilo zogo angelinunua yeye.
😂😄 Au uncle wako atakuwa mimi ila hatujuani humu jf, maana issue ndogo kama hizi huwa simuiti konda, nafanya kumuondoa kibabe upande aliokaa naweka mtu mwingine.
 
🤣🤣🤣 labda mkuu kuna watu ni washari hasa.
 
Issue kama hii haipaswi kutafuta mshindi, inahitajika busara tu kuweza kumaliza mzozo.

Kitendo cha huyo dada kukaidi kuhamia siti nyingine kama alivyoelekezwa na konda wa pili ni dalili ya ukorofi,malezi mabovu na ubinafsi.
Sahih Battling is a sign of Mental illness.
 
Wakuu,

Unaweza kuona kama swali dogo hivi ila ni la msingi sana,kama hujakutana na mgogoro wake basi kuna siku utakukumba tu [emoji3]

Siku kadhaa zilizopita nilipanda basi kwenda mahali fulani,kilichofanya niulize swali ni tukio hili;

Upande wa kushoto dirishani alikaa Mdada umri wa kati tu(25-30).Mimi nilikaa siti ya za upande wa kulia lakini ni kama tulikuwa usawa mmoja tu.

Gari ilianza kuondoka bila shida,tatizo lilianza baada kama ya saa mmoja hivi spidi ikiwa kali ndipo yule dada akafungua dirisha lake ili hewa iingie kwa ajili yake,sasa mara baada ya kufungua haikupita hata dakika moja zikaanza kelele kutoka nyuma yake(siti za nyuma yake na zingine za upande wangu) zikimtaka afunge kioo, alisikia lakini hakufunga,baada ya muda mfupi mmoja wa wanaume waliokuwa siti ya nyuma akafunga kile kioo, Yule Dada akafungua tena,hapo akaambiwa "wewe dada funga hilo dirisha upepo ni mkali sana kuna watoto huku nyuma" yule dada akajibu hata mimi najisikia vibaya nahitaji hewa iingie.

Mzee mmoja wa siti ya nyuma akalifunga lile dirisha kwa nguvu aliporudisha tu mkono dada akafungua tena,mzee akafunga dada akafungua tena huku wale waliokuwa wakilalamika nyuma wakishuhudia[emoji3][emoji28],hapo ikainuka vita Kali balaa kelele za nyuma zikazidi kumshambulia yule dada"huyu dada hana adabu kabisa tunawambia haelewi,kuna watu wana watoto wa miezi sita huku nyuma upepo mkali sana,yule dada akajibu namimi najisikia vibaya kwahio nifanyeje?

Kelele zilipozidi akaja konda wa kwanza"Dada funga hilo dirisha huwezi kusumbua watu wote hawa mtu mmoja"alikuwa anaongea huku anafunga hilo dirisha, (kwa maoni yangu huyu konda alikosa busara)dada akamjibu mimi najisikia vibaya nahitaji hewa ndio maana nimefungua,alipoondoka Konda kuelekea nyuma yule dada akafungua tena dirisha.

Yule konda aliporudi kutoka nyuma akakuta dirisha limefunguliwa tena"we dada naona ni mkorofi tutakushusha"dada akamjibu sawa nishusheni ila mnirudishie nauli yangu yote.

Kelele za kumtaka afunge dirisha hazikwisha, huku wale kinamama wenye vichanga wakimshambulia"wewe hujawahi kuzaa ndio maana huna huruma, huyu hana mtoto ndio maana mjeuri"yule dada akajibu nimeshazaa ila namimi nina matatizo ndio maana nimefungua dirisha.

Kelele zilipozidi akaja konda mwingine (kwa maoni yangu huyu ana busara) akawambia dada ukifungua dirisha lako upepo unawaathiri zaidi walionyuma yako kwahio kama unashida ya hewa naomba nikuhamishie siti nyingine ambayo utaweza kufungua,kule nyuma kuna vichanga"

Siku sikia alijibu nini ila nadhani dada aligoma pia kuhamishwa yule konda akamwacha akaondoka zake.

Basi zoezi la mzee wa siti ya nyuma kufunga na dada kufungua likaendelea baadae mzee akachoka ikabidi aache tu ila lawama za wale kinamama zinaendelea pamoja na wale wanaume wa nyuma(hawa wote lilikuwa lile kabila fulani kubwa kanda ya ziwa) basi wakawa wanasapotiana na kumshutumu yule dada kwa maneno mbalimbali baadae kukawa kimya huku dirisha likiwa wazi mpak mimi niliposhuka kituo fulani nadhani na yule dada alishuka pia pale.

Sasa nauliza wadau,hivi haki za mtu mwenye siti za dirishani ni zipi?Je huyo dada alikuwa sahihi au alikosea?Je ni mhudumu ndio anapaswa kufungua ili kuepusha migigoro kama hii?

Karibu.
Dawa kununua gari lako tu mkuu
 
Back
Top Bottom