Mwenye tatizo kuhusu magari

Mwenye swali au maswali kuhusu Magari ,kuanzia mifumo yote SUSPENSION SYSTEM,COOLING SYSTEM,BRAKE SYSTEM,STEARING SYSTEM ,ENGINE

Uliza hapa ujibiwe
Mkuu Aroon je ni kweli kuwa engine za magari madogo kama vitz, ist, yaani vvti engine ambazo zina cc 1,300 na ambazo ni 2sz haziwezi kufanyiwa overhaul? nauliza hivi maana mafundi wengi ukiwapelekea gari za aina hii mathalani kwenye engine labda kuna kelele sana wao huishia kushauri "kanunue engine nyingine ifungwe, engine za vvti hazifanyiwi overhaul, hata ukifanya ubora wake utakuwa duni sana!
 
Mwenye swali au maswali kuhusu Magari ,kuanzia mifumo yote SUSPENSION SYSTEM,COOLING SYSTEM,BRAKE SYSTEM,STEARING SYSTEM ,ENGINE

Uliza hapa ujibiwe
Niko na gari langu nilikua naendesh mara likazima ghafla Barabarani, wakasema sensor ya pedal imekufa ila wakaunga umeme direct. Nini prospective effects kama sitafunga sensor mapema
 
Usijar mkuu nitakuja kukujibu kitaalamu zaidi,nipo kazin kwa muda huu
 
Na hili wengi mafund wa mtaani hawalijui, zaidi wanabuni au wanahisi tatizo ni VVTI, Ila tatizo la CHECK ENGINE kuwaka huwa ni gas cap kuwa loose hivo hufanya mafuta ku evaporate,

Hivo badilisha kama kimeharibika
Bratha
Bila kuifanyia gari diagnosis mwenyewe n vikamilifu, waezaje jua ni gas cap? Check Engine Light huwaka juu ya gas cap pekee?

Samahani bro, lakini wapotosha kazi na fani inayostahili kuheshimika na kuendelezwa kw ukweli na uungwana.

Ingewezekana kuyatatua matatizo ya magari unavyodai, waunda magari na mifumo wangalikua tayari wana "helplines" hulsusan kuwaskiza wenye magari kw simu tu.

Gari; au hata mifumo kana generator na mifumo mingine, inahusisha mkusanyiko na maunganisho ya sehemu, mifumo na viungo tofauti na kadha wa kadha. Ni upotofu mbaya kudhania waeza jua tatizo bila kuhoji mkusanyiko huu kwa makini.

Nakutolea mfano wa makosa yako:
Umemweleza bro alieuliza swali kuhusu CEL (Check Engine Light) kua tatizo lake ni gas cap. Licha yake kueleza kua diagnosis ilisoma Fault Code ya mfumo wa VVTI - sensor yake, na pia alivyoelezwa kua oil haifanyi mzunguko sawa kwa engine; wewe unasema tatizo ni gas cap.
System ya VVTI hutumia mskumo wa oil kufanya mambo yake (uliyomtajia OP bila kutoa maelezo yeyote kuandamana). Kwa hivyo maelezo ya fundi wake kua mzunguko(mskumo?) wa oil hauko sawa ndio yako sahihi. Issue ya gas cap haiwezi dhuru/tatiza mfumo wa VVTI ila system ya mafuta, na hapa pia inategemea muundo wa system (kama ni return-less fuel circuit) au la.

So kaka, tafadhali, TAFADHALI waacha kuufanya ufundi kua siasa au mchezo. Mengi yako mtandaoni (google) lakini sio kumaanisha google ni chief mechanic.

Ni hayo tu kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro acha kukurupuka, nimeeleza sababu za tatizo lake ,ila nikampa sababu kuu, akishindwa aje

Halafu usikimbilie diagnosis,

Diagnosis inaweza kukupa fault ni flani, ukalifanyia kazi ,tatizo likabaki pale pale kama alivyosema jamaa hapo juu kuhusu pump yake ,tatizo ndio limezidi

Mimi ni mechanical engineer niliyebobea katika Automotive engineering, hivo siongei siasa ndio maana natoa na suluhisho akishindwa aje ,

Tuheshimiane mkuu, hii ni taaluma yangu
 
ni kipi husababisha gari kuwa na mis? gari yangu na mis, naomba msaada! pili, kuna kitu nimeskia kinaitwa fuel treatment , unamwaga kwenye tank LA mafuta, je faida zake ni zipi? na hasara zake ni zipi? na inatumikaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naongezea ,sio kila tatizo la gari lazima ulifanyie Car diagnosis ndio ujue

Matatizo mengine , mtu akiniambia , tayar ubongo unajua shida ni nini, na diagnosis inaweza kukupa fault flan ukaisolve, ndio ukaongeza tatizo kabisa

Hilo tatizo la CHECK ENGINE LIGHT , kwa mujibu wa diagnosis lilivyosoviwa ,tatizo lilibaki pale pale

Lakini wataalamu tunajua kabla hujakimbilia diagnosis na kupoteza hela zaidi, anza na GAS CAP , na kuna sababu za kitaalamu zaidi nimezieleza.
 
Halafu gari halina mfumo unaoitwa GENERATOR ,
 
Mimi engine ya gari langu turbo haifungui ninini shida na itatatuliwaje ni mitsubish L 200
Nakushauri check kama TURBO ACTUATOR PIPE Kama imekazwa vizuri ,angalia hizo rubber pia angalia je haipo loose,
 
Sio kweli kwamba huwez kuifanyia overhaul , ila kuna asilimia kubwa ikapoteza uwezo wake kama wa awali, ndio maana unashauriwa ununue nyingine
 
'... usikimbilie diagnosis, ..'

Nakujibu kw hilo uliotamka.

Ukidai wewe ni 'mechanical engineer' na unatoa mawazo/misimamo kama huo hapo unataka onyesha waunda magari hawayaelewi magari na mifumo waliounda AU wewe ndiwe wajua zaidi yao.
Mfumo ambao unawasiliana na kuangalia mifumo, vifaa na utendakazi ni bure ila wewe bila kuliona gari wacha hata kuliskia linavyoguruma, unajua tatizo?

Aliyekwambia diagnosis machine kazi yake ni kusema tatizo alikupotosha. Code unayoipata pale inakupa mwongozo yaani direction ya kuanzia marekebisho. Kw. mfn. (na hapa najirudia) aliyeuliza swali la VVTI atagundua kua mfumo wa oili ndio wa kuangalia - alivyoambiwa na fundi wake, na sio mambo ya gas cap kama unavyodai wewe. Loose gas cap, for your education and information, haiwezi zua code kwa mfumo wa oil au VVTI, italeta code kwa upande wa fuel system pressure na itasema na kutoa code kuashiria hili. Ni kweli ujuzi na uzoefu ni ya msingi, ndio sababu nayshuku kwako sababu ungelikua kweli 'engineer' unavyotaka tukubali, ungemwambia jamaa aangalie zaidi mfumo wa oil kwa hili ndilo yeyote anayeifahamu VVTI hata kwa vitabu/mtandao angalisema, ni muhimu kuona kua hautoi maelezo ila maneno kuhusu utendakazi.

Jamaa wa GDI uliemwambia tatizo ni pump, kama mafundi walioshindwa kuhoji swala vikamilifu, si amesema pump ya kwanza ilikua bora? Unafahamu tatizo la kwanza la mifumo ya direct injection gasoline iwe GDI, D4 au CGI sio pump ila kifaa kinacho dhibiti(control) mskumo wa mafuta na kw Toyota kinaitwa SCV na waunda gari wamekufanyia marudio Mara kadhaa kuuboresha mfumo mzima?????

So bratha engineer, sio kukurupuka ni kujua ninacho sema.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikweli wapo sahihi, kwa dunia ya sasa FUEL INJECTOR ni bora zaidi kuliko CARBURETOR, hivo kama unaweza fata ushauri wakuweka engine ya FUEL INJECTOR, ili kusolve hizo problem ,ikiwapo ya fuel consuption
 
Nikweli wapo sahihi, kwa dunia ya sasa FUEL INJECTOR ni bora zaidi kuliko CARBURETOR, hivo kama unaweza fata ushauri wakuweka engine ya FUEL INJECTOR, ili kusolve hizo problem ,ikiwapo ya fuel consuption
Ahsante mkuu, km upo Dar naomba namba yako pm tuwasiliane zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu gari halina mfumo unaoitwa GENERATOR ,
Ni wazi hapa kua huelewi unachosema. Nilivyosema ni
' Gari, AU HATA MIFUMO KANA/KAMA GENERATOR NA MIFUMO MINGINE. '
Generator ni mfumo kama vile gari unatumia engine na viungo vingine kama gari, compressor pia ni mfumo.

Pia, kabla ya alternator, magari yalikua yakitumia generators. Nenda uangalie Volkswagen na Mini za miaka ya sitini. Umelijua hilo leo? Alternator, just being technical and precise, is a generator that produces an Alternating Current hence the name Alternator.

Halafu gari halina mfumo unaoitwa GENERATOR ,

Halafu gari halina mfumo unaoitwa GENERATOR ,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bw AROON
Sio kuleta ugomvi au kutafuta maneno. Nisamehe kw kuangazia ninayojua sio sahihi.
Sorry to rock your boat and all the best!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naelewa ulitaka kumaanisha alternator, sasa unazungumzia miaka ya 60s ? Hapa tunazungumzia magari ya kisasa ya karne hii, pia sijaleta ugomvi, kama unataka kuongezea kitu, tumia lugha nzuri. ,
 
Bw AROON
Sio kuleta ugomvi au kutafuta maneno. Nisamehe kw kuangazia ninayojua sio sahihi.
Sorry to rock your boat and all the best!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vema uchangie na usaidie watu kuliko kuleta dharau.

Mimi hapa sipo kuhitaji hata shiling mia ya mtu, nipo kutoa kile kichopo akilini mwangu baada ya kuisomea hii taaluma. ,hivo kama kuna kitu changia sio kuanza KUVURUGA UZI

Haileti maana ,
 
thanks for Ur support, Mungu akubariki! hyo gas treatment naweza kununua na kufanya tu mwenyewe ili kusafisha tank? naomba unieleweshe hapa pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…