Bratha
Bila kuifanyia gari diagnosis mwenyewe n vikamilifu, waezaje jua ni gas cap? Check Engine Light huwaka juu ya gas cap pekee?
Samahani bro, lakini wapotosha kazi na fani inayostahili kuheshimika na kuendelezwa kw ukweli na uungwana.
Ingewezekana kuyatatua matatizo ya magari unavyodai, waunda magari na mifumo wangalikua tayari wana "helplines" hulsusan kuwaskiza wenye magari kw simu tu.
Gari; au hata mifumo kana generator na mifumo mingine, inahusisha mkusanyiko na maunganisho ya sehemu, mifumo na viungo tofauti na kadha wa kadha. Ni upotofu mbaya kudhania waeza jua tatizo bila kuhoji mkusanyiko huu kwa makini.
Nakutolea mfano wa makosa yako:
Umemweleza bro alieuliza swali kuhusu CEL (Check Engine Light) kua tatizo lake ni gas cap. Licha yake kueleza kua diagnosis ilisoma Fault Code ya mfumo wa VVTI - sensor yake, na pia alivyoelezwa kua oil haifanyi mzunguko sawa kwa engine; wewe unasema tatizo ni gas cap.
System ya VVTI hutumia mskumo wa oil kufanya mambo yake (uliyomtajia OP bila kutoa maelezo yeyote kuandamana). Kwa hivyo maelezo ya fundi wake kua mzunguko(mskumo?) wa oil hauko sawa ndio yako sahihi. Issue ya gas cap haiwezi dhuru/tatiza mfumo wa VVTI ila system ya mafuta, na hapa pia inategemea muundo wa system (kama ni return-less fuel circuit) au la.
So kaka, tafadhali, TAFADHALI waacha kuufanya ufundi kua siasa au mchezo. Mengi yako mtandaoni (google) lakini sio kumaanisha google ni chief mechanic.
Ni hayo tu kwa sasa.
Sent using
Jamii Forums mobile app