Changamoto2015
JF-Expert Member
- Oct 1, 2012
- 773
- 314
Huyu bwana yupo kitumbini anakwenda kwa jina MOUSA SUNDRIES P.O BOx 8254 DSM. Plot no. 1306/ 148, kitumbini street.
Ukinunua kitu mfano cha Tsh 2,35000 risiti inaandikwa Tsh 135,000. Hii imetokea baada ya kununua maziwa ya watoto kwake aina ya S26 namba 1. Risiti aliyotoa ni namba 0002/000000966. Tarehe ya manunuzi ni 22.10.2015
Namba ya simu iliyoko kwenye risiti ni 0655255297.
Wana Jf tujitahidi kuwaweka wazi watu kama hawa wanaoibania serikali mapato alafu hao hao ndio wa kwanza kulalamikia serikali imeshindwa ku-perform. Serikali itawezaje ku-deliver kwa uhuni kama huu wa kuibania mapato?
Nenda mahakamani jamaa atapigwa faini
Umejiridhisha kuwa si random error? Maana umetoa mfano mmoja tu ambapo yanaweza kuwa makosa ya kawaida ya kibinadamu. Wewe hiyo risiti uliiangalia pale pale au uliweka tu mfukoni ukaondoka? Nilitegemea utoe mifano ya manunuzi kadhaa ambapo risiti zote zimechakachuliwa, au angalau utoe hint kuwa kuna rafiki zako wawili watatu wamekumbana na hali hiyo kwa huyo mfanyabiashara. Nafahamu watu wanafanya mchezo huo, lakini ulichoeleza hapa bado hakijitoshelezi. (right to be wrong vs right to do wrong)
Sina muda wa kupoteza muda wangu mahakamani, naamini kitengo cha investigation TRA watafanya kazi yao na kumpa onyo huyu mlipa kodi aache mchezo wa kipuuzi! Wafanyabishara waliozoea vya kunyonga kwa serikali hii hawana nafasi watakimbia wote na kuacha wafanyabiashara wakweli ambao ni professionals, innovative na creative kwenye soko. Hawa makanjanja waliozoea ujanja ujanja wataondoka wenyewe maadam jipu limepata mkamuaji.
duh watu wana roho mbaya!!yaani we kununua kitu kimoja ukapewa risiti tena moja tayari akili yako imekutuma kumshutumu hujui error maana yake nn?au umefanyiwa mara ngapi
Mkuu wenye kuweza kupata details kama ni tukio moja au ndio mchezo wake endelevu ni investigators wa TRA na sio mimi mnunuzi. Pili, akiona bandiko hili na kama ndio mchezo wake naamini atapata hofu na kuacha mara moja kabla balaa halijamshukia. Tatu, siwezi tena kwenda kununua kitu kwenye duka ambalo unajua kabisa unamfaidisha mmiliki badala ya kodi kwenda serikalini ikafanye huduma za kijamii - kwa hivyo keshanipoteza kama mteja.
Mwingine ni super market iliyopo tegeta kibaoni upande wa kulia kama unaelekea wazo hill, huyu jamaa anakupa risiti ya EFD lakini kitu cha ajabu pale kwenye VAT unakuta pameandikwa 0Tsh Kama zile risiti za sheli ya mafuta. Nilishawahi kwenda kumripoti katika ofisi za TRA pale kibo complex lakini naona mchezo wake huo bado unaendelea. Nadhani anatumia mashine ya petro station ili kukwepa kodi ya VAT
Hili ipu kweli kweli. Nilikuwa nataka kujiuliza supermarket wanawezaje kufanya hivyo, kumbe zipo mbinu nyingi! Aisee! Kama ulimripoti enzi za zama zile, usitegemee kama kuna ambalo lingeweza kutokea,sana sana uliwatengenezea dili hao jamaa wa TRA maana uliwapa tool kwa ajili ya kum-blackmail na wala si vinginevyo. Nina hakika sasa hali inaweza kuwa tofauti, angala kwa kipindi hiki so far.Mwingine ni super market iliyopo tegeta kibaoni upande wa kulia kama unaelekea wazo hill, huyu jamaa anakupa risiti ya EFD lakini kitu cha ajabu pale kwenye VAT unakuta pameandikwa 0Tsh Kama zile risiti za sheli ya mafuta. Nilishawahi kwenda kumripoti katika ofisi za TRA pale kibo complex lakini naona mchezo wake huo bado unaendelea. Nadhani anatumia mashine ya petro station ili kukwepa kodi ya VAT
Mkuu hawa watu ni kuwaweka wazi tu! Wezi wengine wapo humu humu JF wanateteana sijui random errors sijui kitu gani. Kama ni random errors watamalizana na investigators wa TRA.