Mwenye uelewa gari langu linapandisha temperature katika engine

Magita

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
319
Reaction score
144
Yapata miezi mi3 sasa gari langu linatatizo ya engine kupandisha joto, ni Toyota spacio hii ilitokea baada ya kubadilisha rejeta ikawa unapotembea kama umbali wa 45 au 40km unaona inatokea alarm ya high temperature ktk dash board.

Nikaipeleka kwa fundi tena akasema tubadilishe mfuniko wa rejeta ok tukabadilisha tatizo likawa linaendelea, nikampelekea tena akasema tubadilishe sensor ya temperature ok tukabadilisha lakni tatizo bado linaendelea sasa.

Je mwenye ujuzi gari langu lina tatizo gani?
 
Angalia themostat, au angalia kama rejeta haijatoboka ikavujisha maji

Kwa ujumla angalia mfumo wa kupoza injini ambao una mifumo miwili,mfumo wa maji na wa oil
 
Pia angalia kama mzunguko wa maji katika injini uko sawa hasa water pump,na pia kagua kama rejeta haiko clogged labda na matope,au kama mzunguko wa oil uko sawa hasa oil filter kama ni nzuri /pump kama haina tatizo,kwa ujumla angalia cooling system

Themostat inatakiwa kufunguka kuruhusu maji yaingie kupoza injini na kufunga,kama ina tatizo la kujifungua kuruhusu maji ya kupoza engine basi lazima itachemsha,

Jipoge pige uende kwenye gereji nzuri kabla hujaunguza injini
 
Angalia vitu vitano vifuatvyo:-
1. Fan belt
2. Coolant unayotumia
3. Radiator kama haivuji au zile airspace za radiator kama zimeziba ipeleke gari carwash ikaoshwe na high pressure pump
4. Propeller
5. Control box ya umeme wa gari
 
Ng'oa hiyo rejeta tupa kule.. Ni kimeo kitakacho kuulia engine ukikiendekeza...
 
Njoo Gereji Tabata Dampo Kwa matengenezo ya magari,matenk ya Mafuta,bodi za magari nk 0756627204
 
Mkuu naona umeeleza kuwa kuwa tatizo limeanza baada ya kubadili radiator,lakini hukusema kwa nini ulibadili radiator iliyokuwepo maana inaonekana kama umetoa radiator iliyokuwa inafanya kazi ukaweka kimeo. Pili inawezekana ukawa ni wakati muafaka wa kumfanyia assessment huyo fundi wako kabla spacio haijakaa juu ya mawe maana huu mshiko wa mwendokasi si mchezo.
 
Hili tatizo limeeanza baada ya kubadilia Radiator, Radiator niliibadilisha baada ya kutobolewa na fan. Gari niliingiza ktk shimo/bwawa lenye maji mengi so gari ikazama yote ktk ile sehemu ya mbele matokeo yake fan ikakatika na ikatoboa ile Radiator
 
Na mkisema fan haizunguki sio kweli maana kama naiendesha hii baada ya kutembea kama 25 hadi 35km ndio ile alama ya high temp. inatokezaga ikitoka tu naweka gari pembeni na nikifungua bonet fan inaendelea ku cool
 
Na ukisema Radiator inavujisha maji sio kweli cos ukiangalia maji ktk radiator bado unakuta is FULL
 
Unakaanga engine sasa hivi.angalia oil , check engine, stop driving. Ipeleke hospitali sasa hivi.
 
Pole kaka, utatuzi ni huu , kwanza usije thubutu kupiga horn wakati gari ipo ktk gia namba 4, pili kabla ya kuwasha gali kwanza tena mate kidogo chini na mwisho kilabunapoeudi reverse washa weiper japo kidogo mkuu
 
Pole sana mkuu.huna haja ya kuhangaika na kutafuta tiba hapo kwa uelewa wangu kulingana na maelezo yako shida au utatuzi upo sehem mbili tuu.

Kwanza kwenye upande wa rejeta.

Hapo yaweza kuwa rejeta iliyoweka ni kimeo.
Inaweza ikawa baadhi ya njia zimeziba,au rejeta yenyewe chafu kwa nje so inazuia hewa kupita vizuri,au imepukutika kwa nje.


Fan ya kupooza.kwa kuwa hiyo gari inatumia fen ya umeme na umesema kuwa chanzo cha rejera kutoboka ni baada ya panga la fen kukatika ndio likatoboa rejeta hivyo ulibadilisha kuna mambo haya ya kuzingatia.

Aidha kama ni panga peke yake ndio ulibadili unaweza ukawa umeweka tofauti au lina panga chache??.

Au mota yenyewe ni tofauti na ya mwanzo hapo kama ulibadilisha na mota.

Mwisho angalia kama ulibadili mota usije ukawa umeiinga kinyume. Baada ya kuvuta hewa nje kutoka mbele ya gari kuingiza ndani yenyewe inatoa hewa ya joto ndani na kuipuliza nje hivyo hewa ya joto badala ya kuyapooza maji inayapasha moto.

Ukitaka kufaham juu ya mzunguko wa feni kama upo sahihi basi.washa gari feni ikiwa inazunguka chukua kipande cha karatasi weka mbele ya rejeta or condeser ya ac hapo inatakiwa karatasi ivutiwe ndani itanasa ukiona inadondoka ujue fen inazunguka kinyume.



Swali ulibadilisha na fen?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…