Ipo pembezoni kidogo uelekeo wa old shinyanga....eneo linaitwa butengwa.
Ukitoka stendi kuu ya shinyanga (manyoni) chukua usafiri Kama ni bajaji au pikipiki za kukodi waambie wakupeleke butengwa kupitia barabara ya old shinyanga halafu halafu wakunje kulia barabara inayoelekea machinjio ya kisasa..shule haiko mbali na barabara ya ya lami ni Kama kilometa mbili na kidogo hivi kabla ya kufika machinjio ya kisasa.
Ukitoka stendi kuu utanyooka na barabara Hadi sheli ya Mo oil utakunja kushoto kuiacha barabara ya mwanza na kuifuata barabara ya old shinyanga, utapita maeneo ya ofisi za ccm wilaya, junction ya mdaduka mengi/stend ya zamani, Japanese corner,stend ya old shinyanga opposite na Kota za polisi,soko la majengo,njiapanda shy park,idara ya maji, bushushu, mwishoni mwa bushushu utaona barabara kubwa ya vumbi imekatisha kulia kwako utaifuata hiyo kwa zaidi ya km 2 utaoiona shule ikiwa na mabati ya kijani, ni shule kubwa nzuri sana kimiundombinu ....
Ni shule mpya bado haijafahamika na wenyeji wengi, usishangazwe na kutojulikana na wenyeji wa pale mjini...kimiundombinu imejitosheleza.